-
Mahakama ya Katiba Zimbabwe yaanza kusikiliza kesi kuhusu uchaguzi wa rais
Aug 22, 2018 03:23Mahakama ya Katiba nchini Zimbabwe inaanza kusikiliza leo, kesi ya chama kikuu cha upinzani MDC kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi rais Emmerson Mnangangwa.
-
Rais Mnangagwa awataka Wazimbabwe kusonga mbele baada ya machafuko ya uchaguzi
Aug 13, 2018 22:47Rais Emmerson Mnangangwa wa Zimbabwe jana alisema kuwa Wazimbabwe wanapaswa kuwa kitu kimoja ili kujenga uchumi wa nchi yao na kuwenda kando kipindi cha uchaguzi. Watu sita waliuawa katika ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi wa rais huko Zimbabwe mwezi huu.
-
Hafla ya kuapishwa Rais wa Zimbabwe yaakhirishwa ili kusubiri uamuzi wa kesi ya wapinzani
Aug 11, 2018 09:55Hafla ya kuapishwa Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye alishinda katika uchaguzi wa Julai 30 imeakhirishwa baada ya wapinzani kuwasilisha kesi mahakamani wakipinga matokeo ya uchaguzi huo.
-
Chamisa awasilisha hoja mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi Zimbabwe
Aug 10, 2018 23:33Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa jana Ijumaa aliwasilisha mahakamani hoja ya kupinga ushindi wa Rais Emmerson Mnangagwa katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni nchini humo.
-
Wapinzani waendelea kulalamikia matokeo ya uchaguzi Zimbabwe
Aug 09, 2018 03:25Wapinzani nchini Zimbabwe wamendelea kufanya maandamano wakilalamikia matokeo ya uchaguzi wa Rais wa hivi karibuni yaliyompa ushindi Emmerson Mnangagwa wa chama tawala cha ZANU-PF.
-
Wafuasi 28 wa upinzani Zimbabwe washtakiwa kwa kuzusha vurugu baada ya uchaguzi
Aug 05, 2018 03:45Wafuasi wasiopungua 28 wa mrengo wa upinzani nchini Zimbabwe wamepelekwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya kuzusha vurugu na machafuko baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuu.
-
Rais mpya wa Zimbabwe na changamoto anazokabiliana nazo
Aug 04, 2018 22:02Emmerson Mnangagwa amechaguliwa kuwa rais wa Zimbabwe katika uchaguzi wa kwanza ambao haukumuhusisha rais wa kwanza wa nchi hiyo Robert Mugabe aliyetawala nchi hiyo kwa muda wa miaka 37. Baada ya kutangazwa matokeo rasmi ya uchaguzi huo wa Jumatatu nchi hiyo imetumbukia katika ghasia za kisiasa huku wapinzani wakidai kuwepo wizi wa kura.
-
Upinzani, fujo na machafuko yaendelea baada ya uchaguzi nchini Zimbabwe.
Aug 04, 2018 11:21Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe ameyakataa matokeo ya uchaguzi wa rais akisema ni ya "uongo".
-
Rais wa Zimbabwe asisitiza udharura wa kudumisha umoja kufuatia ghasia
Aug 04, 2018 03:43Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametoa wito kwa wananchi kudumisha umoja kufuatia ghasia zilizoibuka baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza mshindi katika uchaguzi uliofanyika wiki hii.
-
Rais Emmerson Mnangagwa atangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais Zimbabwe
Aug 02, 2018 23:55Tume ya Uchaguzi nchini Zimbabwe, imemtangaza asubuhi ya leo Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika siku ya Jumatatu iliyopita.