Rais wa Zimbabwe asisitiza udharura wa kudumisha umoja kufuatia ghasia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47221-rais_wa_zimbabwe_asisitiza_udharura_wa_kudumisha_umoja_kufuatia_ghasia
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametoa wito kwa wananchi kudumisha umoja kufuatia ghasia zilizoibuka baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza mshindi katika uchaguzi uliofanyika wiki hii.
(last modified 2024-06-10T09:25:34+00:00 )
Aug 04, 2018 08:13 UTC
  • Rais wa Zimbabwe asisitiza udharura wa kudumisha umoja kufuatia ghasia

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametoa wito kwa wananchi kudumisha umoja kufuatia ghasia zilizoibuka baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza mshindi katika uchaguzi uliofanyika wiki hii.

Hadi sasa watu sita wamepoteza maisha baada ya matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumatatu kuoneysha kuwa Rais Mnagagwa ameshinda uchaguzi wa rais na chama chake cha Zanu-PF nacho pia kimepata ushindi katika uchaguzi wa bunge.

Kwa mujibu wa Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Zimbabwe (ZEC), Mnangagwa ameshinda kwa kupata aslimia 50.8 ya kura zote dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa kutoka MDC aliyepata asilimia 44.3 ya kura zote.

Katika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mnangagwa amesema: "Huu ni mwanzo mpya na tunapaswa kuungana. Tumepata ushindi kwa uadilifu na uwazo na hakuna chochote cha kuficha."

Wanajeshi wa Zimbabwe wakikabiliana na wafuasi wa upinzani wanaopinga matokeo ya uchaguzi

Nayae Chamisa amesema atatumia vyombo vya sheria kupinga matokeo ya uchaguzi ili kulinda matakwa ya wananchi.

 Mnangagwa  ameshinda Urais wa Zimbabwe katika uchaguzi wa kwanza wa Urais, baada ya Robert Mugabe kuondolewa madarakani mwezi Novemba mwaka 2017.