Mbunge wa Uganda Bobi Wine kufikishwa katika mahakama ya kijeshi leo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47625-mbunge_wa_uganda_bobi_wine_kufikishwa_katika_mahakama_ya_kijeshi_leo
Mbunge wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi kwa jina maarufu Bobi Wine leo anatarajiwa kurudishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 23, 2018 04:47 UTC
  • Mbunge wa Uganda Bobi Wine kufikishwa katika mahakama ya kijeshi leo

Mbunge wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi kwa jina maarufu Bobi Wine leo anatarajiwa kurudishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa hiyo imewashtua mawakili wake ambao awali walijulishwa kwamba, kesi ya Mbunge huyo wa upinzani ambaye pia ni msaani wa muziki itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa mjini Kampala.

Wakili wa Bobi Wine anasema kuwa mteja wake ameteswa sana na jeshi, lakini jeshi kwa upande wake linakana madai ya kuteswa Mbunge huyo. Bobi Wine anatarijiwa kufikishwa mahakamani akituhumiwa kumiliki silaha kinyume na sheria.

Jeshi ambalo ndilo linalomshikilia Bobi Wine kwa tuhuma za kuchochea ghasia linasema kuwa hajateswa na Rais Yoweri Museveni ametupilia mbali madai ya kuteswa Mbunge huyo na kuzitaja kuwa habari za uongo.

Robert Kyagulanyi ( Bobi Wine)

Wakati huo huo, mashirika na asasi mbalimbali za kutetea haki za binadamu zimeendelea kupaza sauti zikitaka kuachiliwa huru Mbunge huyo na Wabunge wengine wa upinzani.

Aidha baadhi yya Wabunge wa Kenya wamesema kuwa, wataelekea Kampala na kufanya maandamano endapo serikali ya Rais Museveni haitamuachilia huru Bobi Wine katika kipindi cha juma moja.

Katikka upande mwingine kampeni ya kutakka kuachiliwa huru Mbunge huyo wa upinzani nchini Uganda zimechukua wigo wa kimataifa.

Baadhi ya watu mashuhuri akiwemo mwandishi mkongwe wa Nigeria Wole Soyinka na wanamuziki wamejiunga na kampeni ya kutaka kuachiliwa huru Mbunge huyo wa jimbo la Kyadondo Mashariki  Robert Kyagulanyi au Bobi Wine.