-
Uganda kutoa mafunzo ya kijeshi ya miezi sita kwa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Afrika ya Kati
Sep 05, 2025 23:34Jeshi la Uganda UPDF litatoa mafunzo ya kijeshi ya muda wa miezi sita kwa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Afrika Kati katika hatua ya kuisadia nchi hiyo kujenga upya jeshi lake baada ya miaka ya mingi ya kuvurugika kwa amani na utulivu nchini humo.
-
UN yaonya kuhusu uwezekano wa uhalifu wa kivita na dhidi ya binadamu DRC
Sep 05, 2025 23:31Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza Ijumaa kwamba makundi yenye silaha pamoja na vyombo vya dola katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), yamehusika katika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaoweza kufikia kiwango cha uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.
-
Maulidi ya Mtume SAW yaadhimishwa kwa sherehe kubwa Somalia, yatangazwa sikukuu rasmi ya kitaifa
Sep 05, 2025 11:15Maelfu ya Waislamu nchini Somalia jana Alkhamisi, waliandamana mitaani katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu kuadhimisha siku aliyozaliwa Bwana Mtume Muhammad SAW, huku Wizara ya Kazi na Masuala ya Kijamii ikiitangaza kuwa ni sikukuu ya kitaifa na siku rasmi ya mapumziko kuadhimisha tukio hilo.
-
DRC yatangaza mripuko wa 16 wa Ebola; WHO yatoa indhari
Sep 05, 2025 07:08Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza mripuko mpya wa Ebola katika jimbo la kati la Kasai, ambalo ni la 16 nchini humo tangu 1976, huku Shirika la Afya Duniani (WHO) likitahadharisha kuwa huenda maambukizi ya maradhi hayo yakaongezeka.
-
Watu wa Afrika walaani jinai za utawala wa Israel dhidi ya Yemen na Gaza
Sep 05, 2025 06:54Wananchi wa nchi kadhaa za Afrika wamefanya maandamano makubwa kulaani jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Yemen na Gaza, wakionesha mshikamano wa wazi na harakati za ukombozi wa Wapalestina.
-
Afrika CDC: Mpox bado ni dharura ya kiafya barani Afrika
Sep 05, 2025 03:34Ugonjwa wa Mpox ambao umeenea katika nchi za Kiafrika na kuua mamia ya watu, bado ni dharura ya kiafya katika bara hilo. Taarifa hii imetolewa na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Barani Afrika (Africa CDC).
-
Mjukuu wa Mandela: Mateso ya Waafrika Kusini weusi chini ya apartheid si lolote ikilinganishwa na masaibu ya Wapalestina
Sep 05, 2025 00:20Mjukuu wa kiongozi wa mapambano ya ukombozi wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela, Mandla Mandela, amelaani mzingiro wa utawala wa Israel na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo dhidi ya watu wa Palestina, akisema kwamba mateso yanayowapata Wapalestina chini ya utawala vamizi wa Israel ni mabaya zaidi kuliko yale yaliyowapata Waafrika Kusini weusi chini ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
-
Njaa yaongezeka nchini Nigeria sambamba na kupungua usambazaji wa chakula
Sep 04, 2025 22:53Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema watu milioni 31 wanakabiliwa na uhaba wa chakula nchini Nigeria, hasa kaskazini mashariki, ambako watu milioni 2.3 wamelazimika kuacha makazi na mashamba yao katika kipindi cha miaka 15 ya vita.
-
Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Zambia ahukumiwa kifungo cha miaka 4 jela kwa ufisadi
Sep 04, 2025 09:44Mahakama ya Zambia leo Alhamisi imemhukumu Joseph Malanji aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kifungo cha miaka minne jela na kazi ngumu kwa kupatikana na hatia ya ufisadi.
-
Ajali nyingine ya boti yaua watu zaidi ya 60 nchini Nigeria
Sep 04, 2025 04:13Kwa akali watu 60 wamefariki dunia baada ya mashua iliyokuwa imebeba zaidi ya abiria 100 kupinduka na kuzama katika jimbo la Niger, kaskazini mwa Nigeria.