-
Watu 24 wauawa katika mashambulizi ya waasi wa RSF magharibi mwa Sudan
Aug 28, 2025 08:15Watu wasiopungua 24 wameuawa na wengine 55 kujeruhiwa kutokana na mashambulizi ya makombora ya waasi wa RSF katika mji mkuu wa El-Fasher, kaskazini mwa Darfur, magharibi mwa Sudan.
-
Afrika Kusini: Mauaji ya Wapalestina yameongezeka sana, Israel inapaswa kusitisha vita
Aug 28, 2025 08:11Afrika Kusini imesema mauaji ya Wapalestina yanazidi kuongezeka na hivyo imeutaka utawala wa Israel uafiki mkataba wa kusitisha mapigano uliojadiliwa na wadau wote muhimu.
-
Niger yalipiza kisasi, yaweka masharti magumu kwa wasafiri kutoka nchi za Ulaya
Aug 28, 2025 08:04Kufuatia sheria mpya ya usafiri iliyowekwa na serikali ya Niger, raia wa nchi zilizoathirika sasa inawalazimu wawasilishe maombi yao ya visa katika balozi za Niger zilizoko Russia, Uswisi, na Uturuki.
-
Mwanaharakati mtetezi wa haki Kenya atangaza kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha urais 2027
Aug 28, 2025 02:37Mwanaharakati maarufu wa kutetea haki nchini Kenya Boniface Mwangi ametangaza kwamba atawania urais katika uchaguzi mkuu wa 2027.
-
Kinshasa na M23 waanza tena mazungumzo Qatar katika juhudi za kutekeleza makubaliano ya kusitisha vita
Aug 27, 2025 07:19Duru mpya ya mazungumzo kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23 inaendelea katika mji mkuu wa Qatar, Doha. Pande hizo mbili zinatazamia kufikia makubaliano juu ya namna ya kutekeleza mapatano waliyosaini mwezi uliopita kwa upatanishi wa Qatar.
-
Rais wa Sudan Kusini atuhumiwa kwa upendeleo baada ya kumteuwa binti yake katika cheo cha juu serikalini
Aug 27, 2025 07:10Adut Salva Kiir, binti wa Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ameteuliwa na baba yake kuwa Mjumbe wa Rais Anayehusika na Mipango Maalumu, kazi ambayo awali ilikuwa inafanywa na Makamu wa Rais wa sasa.
-
Ufaransa yarejesha mafuvu ya vichwa Madagascar miaka 127 baada ya mauaji ya kikoloni
Aug 27, 2025 03:29Ufaransa jana Jumanne ilirejesha mafuvu matatu nchini Madagascar, likiwemo moja linaloaminika kuwa la mfalme aliyekatwa kichwa na wanajeshi wa Ufaransa kufuatia mauaji ya Agosti 1897.
-
Baraza la Mawaziri Sudan lafanya kikao cha kwanza mjini Khartoum tangu 2023
Aug 27, 2025 03:28Baraza la Mawaziri la Sudan ya Sudan lilifanya mkutano wake wa kwanza katika mji mkuu, Khartoum, jana Jumanne tangu kuzuka kwa vita vya ndani nchini humo katikati ya Aprili, 2023.
-
Mrengo wa upinzani Somalia wafikia makubaliano na serikali kuhusu uchaguzi
Aug 26, 2025 22:58Mrengo uliojitenga na muungano mkuu wa upinzani nchini Somalia wa Salvation Forum umetia saini makubaliano ya uchaguzi na Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, na hivyo kutoa pigo kubwa kwa harakati kuu ya upinzani nchini humo.
-
Ugonjwa wa kipindupindu wauwa watu 63 mashariki mwa Chad
Aug 26, 2025 22:57Watu wasiopungua 63 wamepoteza maisha kwa ugonjwa wa kipindupindu katika jimbo la Ouaddai mashariki mwa Chad tangu katikati ya mwezi Julai mwaka huu. Taraifa hii imetolewa na Wizara ya Afya ya nchi hiyo.