-
Wanahabari Nigeria walaani mauaji ya waandishi wenzao huko Gaza
Aug 18, 2025 03:13Muungano wa Waandishi wa Habari wa Nigeria (NUJ) umelaani vikali mauaji ya wanahabari yaliyofanywa na utawala ghasibu wa Israel huko Gaza na kusisitiza kuwa, hujuma hizo za utawala wa Kizayuni dhidi ya waandishi wenzao katu haziwezi kuwazuia wahudumu wa tasnia hiyo kuendelea kufichua ukweli.
-
Madaktari wa Sudan: RSF imeua watu wengi kwenye kambi ya Abu Shouk, wamo watoto saba
Aug 17, 2025 23:56Mtandao wa Madaktari wa Sudan umeripoti kuwa, wapiganaji wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) wamefyatua makombora kwenye kambi ya wakimbizi waliokumbwa na njaa katika eneo la magharibi mwa Darfur na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 31 wakiwemo watoto saba na mwanamke mjamzito.
-
DRC yapinga kupelekwa balozi mdogo wa Kenya mjini Goma
Aug 17, 2025 08:07Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepinga hatua ya Kenya ya kumteua balozi mdogo anayetazamiwa kutumwa katika mji wa Goma ulioko mashariki mwa DRC, ikiuelezea uamuzi huo kuwa "usiofaa".
-
Tanzania, Burundi zazindua ujenzi wa reli ya SGR Uvinza-Musongati
Aug 17, 2025 00:22Mataifa mawili Jirani ya Tanzania na Burundi yamezindua ujenzi wa reli ya SGR Uvinza-Musongati.
-
Ramzy Abou Ibrahim aapa kulitetea taifa lake la Palestina
Aug 16, 2025 22:56Ramzy Abou Ibrahim, mkuu wa Jumuiya ya Wapalestina nchini Nigeria, amesema kuwa, Wapalestina kamwe hawatasalimisha ardhi yao licha ya uvamizi wa Israel, huku wakitetea kwa dhati haki ya Hizbullah ya kumiliki wa silaha dhidi ya vikosi vinavyokalia kwa mabavu.
-
Kenya yalaumiwa kwa kupuuza ripoti ya dhulma kwa watoto
Aug 16, 2025 07:47Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International, limemshtumu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Kipchumba Murkomen kwa kupuuza uchunguzi uliofanywa na shirika moja kuhusu ulanguzi wa watoto nchini humo.
-
AU yataka ulimwengu utumie ramani ya dunia inayoakisi ukubwa halisi wa bara la Afrika
Aug 16, 2025 01:38Umoja wa Afrika (AU) umeunga mkono kampeni inayolenga kukomesha matumizi ya ramani ya dunia ya karne ya 16 ya Mercator, inayotumiwa na serikali na mashirika ya kimataifa, na badala yake kutumia ramani inayowakilisha kwa usahihi zaidi ukubwa wa bara la Afrika.
-
Wanigeria wafanya matembezi ya amani ya Arubaini ya Imam Hussein (as) na kutangaza mshikamano na Gaza
Aug 15, 2025 22:52Maelfu ya waombolezaji wa Nigeria wamekamilisha matembezi ya kinembo ya siku mbili ya kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein (as) na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa Wapalestina.
-
Anayedaiwa kuwa jasusi wa Ufaransa akamatwa kwa madai ya njama ya mapinduzi ya Mali
Aug 15, 2025 22:51Watawala wa kijeshi wa Mali wametangaza kuwa wamemkamata raia mmoja wa Ufaransa kwa tuhuma za kufanya ujasusi wa nchi yake katika jaribio la kuliyumbisha taifa hilo la Afrika.
-
Zaidi ya watu milioni nne wanakabiliwa na baa la njaa Somalia
Aug 15, 2025 07:21Idadi ya watu wanaokabiliwa na baa la njaa nchini Somalia inazidi kuongezeka katika nchi hiyo inayokabiliwa na ukosefu wa amani kutokana na harakati za kundi la kigaidi la al-Shabab.