-
Zaidi ya watu 200 wamefariki DRC kwa maporomoko kwenye mgodi unaodhibitiwa na waasi
Jan 31, 2026 23:00Watu wasiopungua 200 wameaga dunia mapema wiki hii wakati mvua kubwa iliposababisha mfululizo wa maporomoko ya udongo katika mgodi wa madini ya koltani ulioko Rubaya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, eneo ambalo tangu mwaka 2024 liko chini ya udhibiti wa kundi la waasi la M23.
-
Niger yasema Ufaransa imehusika na shambulio la kigaidi katika uwanja wa ndege wa Niamey
Jan 31, 2026 09:25Kiongozi wa mpito wa Niger, Jenerali Abdourahamane Tchiani, ameituhumu Ufaransa pamoja na nchi jirani za Benin na Ivory Coast kwa kufadhili shambulio la kigaidi lililolenga uwanja mkuu wa kimataifa wa ndege katika mji mkuu wa taifa hilo la Sahel mapema Alhamisi.
-
Mkuu wa AU aeleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka mivutano katika eneo la Tigray, Ethiopia
Jan 30, 2026 23:23Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika jana Ijumaa alitoa wito kwa pande zinazozozana kujiepusha na mivutano haraka iwezekanavyo baada ya vyombo vya habari kuripoti kwamba safari za ndege zimesimamishwa katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia kutokana na mapigano ya silaha yaliyoibuka katika eneo hilo.
-
UNICEF: Mgogoro mkubwa zaidi duniani: Sudan ina wakimbizi wa ndani milioni 9.5
Jan 30, 2026 23:12Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) amesema kuwa Sudan imekumbwa na mgogoro mkubwa zaidi wa wakimbizi wa ndani duniani, huku takriban watu milioni 9.5 wakilazimika kuhaka makazi yao katika majimbo 18.
-
Mjadala mkali waibuka baada ya jeshi la Uganda kuutuhumu ubalozi wa Marekani kumficha Bobi Wine
Jan 30, 2026 07:19Jenerali Muhoozi Kainerugaba, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Uganda (UPDF), , amezua mjadala mkubwa baada ya kuutuhumu ubalozi wa Marekani nchini humo kwa kumficha kiongozi wa upinzani Bobi Wine.
-
Burkina Faso yavunja vyama vyote vya siasa, yasema vimechochea migawanyiko
Jan 30, 2026 04:16Serikali ya Burkina Faso inayoongozwa na jeshi imetoa amri ya kuvunjwa vyama vyote vya siasa ambavyo kabla ya hapo vilikuwa tayari vimelazimishwa kusimamisha shughuli zao kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini humo miaka minne iliyopita.
-
IOM: Hali mbaya ya usalama imelazimisha mamia ya Wasudan kuhama makazi yao Kordofan Kusini
Jan 30, 2026 04:15Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza kuwa watu wasiopungua 285 ni miongoni mwa wale waliolazimika kuyahama makazi yao kwenye kipindi cha siku mbili za karibuni katika miji ya Kadugli na Al-Kuwaik iliyoko kwenye Jimbo la Kordofan Kusini nchini Sudan kutokana na hali mbaya ya usalama.
-
Somalia yamteua mkuu mpya wa jeshi kuchukua nafasi ya Jenerali Rage
Jan 29, 2026 23:19Baraza la Mawaziri la Somalia limemteua Brigedia Jenerali Ibrahim Mohamed Mohamud kuwa Kamanda mpya wa Jeshi la Taifa la Somalia (SNA). Hii ni kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Somalia iliyosomwa na msemaji wa serikali, Abdinasir Ahmed Bashir.
-
Shirika la Ndege la Ethiopian Airlines limefuta safari zake kwenda Tigray kwa sababu ya mapigano
Jan 29, 2026 23:18Shirika la ndege la Ethiopian Airlines limefuta safari za ndege kuelekea kaskazini mwa mkoa wa Tigray baada ya mapigano ya silaha kuzua hofu ya kuibuka mzozo mpya katika eneo hilo.
-
Juhudi za uokoaji zinaendelea Msumbiji baada ya wiki kadhaa za mvua kubwa
Jan 29, 2026 09:10Juhudi za utafutaji na uokoaji zinaendelea kufanywa nchini Msumbiji baada ya wiki kadhaa za mvua kubwa iliyosababisha mafuriko makubwa, kuzamisha ardhi ya mashamba, kubomoa nyumba na miundombinu kujaa maji.