-
Shura ya Maimamu Tanzania yakaribisha kuachiwa huru Masheikh 12
Mar 05, 2025 10:12Shura ya Maimamu Tanzania imepokea kwa mikono miwili uamuzi wa mahakama wa kuwaachia huru Masheikh 12 waliokaa gerezani miaka 10, (2015-2025), kwa tuhuma za ugaidi. Uamuzi huo umetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Arnold John Kirekiano.
-
Uingereza yakataa kuilipa Rwanda fidia baada ya kufuta mkataba wa wahamiaji
Mar 05, 2025 06:46Serikali ya Uingereza imekataa kuilipa Rwanda fidia baada ya kufuta mkataba wa wahamiaji kati ya nchi hizo mbili.
-
Wasomali wengine milioni moja kuathiriwa na ukosefu wa usalama wa chakula kutokana na ukame
Mar 05, 2025 02:50Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeripoti kuwa Ukame, mzozo na kupanda kwa bei za vyakula vinaweza kusabaisha uhaba na kukosekana usalama wa chakula kwa Wasomali wengine milioni moja katika miezi mingine ijayo.
-
Mkuu wa WHO: Uongozi wa Kiafrika uko imara katika nyanja nyingi za afya duniani
Mar 05, 2025 02:43Tedros Adhanom Ghebreyesus Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amebainisha kuwa uongozi wa Afrika una nguvu katika nyanja nyingi za afya duniani.
-
Wahamiaji 349 walizuiwa kuendelea na safari katika pwani ya Libya wiki iliyopita
Mar 05, 2025 00:43Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) lilisema jana Jumanne kwamba wahamiaji 349 walizuiwa kuendelea na safari nje ya pwani ya Libya wiki iliyopita.
-
Umoja wa Mataifa: Waasi wa M23 wawateka wagonjwa 130 mashariki mwa DRC
Mar 05, 2025 00:41Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, wapiganaji wa M23 wamewateka karibu watu 130 kutoka hospitali za mji wa Goma wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, unaodhibitiwa na waasi hao.
-
Rwanda: Serikali ya Uingereza imevunja uaminifu
Mar 04, 2025 08:16Serikali ya Rwanda imeishutumu Uingereza kwa kile ilichokita kuwa kuvunja uaminifu na kuchukua hatua zisizo na msingi dhidi ya Kigali, na imeitaka serikali ya Uingereza iilipe Rwanda kiasi cha pauni milioni 50 chini ya mpango wa Ushirikiano wa Wahamiaji na Maendeleo ya Kiuchumi ambao haupo kwa sasa.
-
Wabunge wa Ghana wawasilisha mswada wa kuongeza adhabu kwa wapenzi wa watu wa jinsia moja
Mar 04, 2025 07:55Wabunge wa Ghana wamewasilisha tena mswada dhidi ya mahuusiano ya kiimapenzii ya watu wa jinsia moja (LGBTQ), baada ya jaribio la awali kushindikana kwa sababu ya changamoto za kisheria.
-
Umoja wa Mataifa: Watoto wa mwaka mmoja ni miongoni mwa waliobakwa Sudan
Mar 04, 2025 07:44Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, watu wenye silaha wanabaka na kuwanyanyasa kingono watoto wenye umri hadi mwaka mmoja katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan.
-
Kenya nayo yajiandaa kukabiliana na ugonjwa usiojulikana
Mar 03, 2025 23:29Wizara ya Afya nchini Kenya imetangaza kuwa, imo mbioni kupambana na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana ambao umeathiri zaidi ya watu 200 katika vijiji vitatu vya jimbo la Kisii eneo la Nyanza Magharibi ya nchi hiyo.