-
Rwanda: Aliyekuwa mkuu wa Kitivo cha Tiba cha Butare ashtakiwa Paris kwa Mauaji ya Kimbari
Mar 03, 2025 23:29Mkuu wa zamani wa Kitivo cha Tiba cha Butare nchini Rwanda ameshtakiwa mjini Paris Ufaransa kwa mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya binadamu na kula njama ya kutenda uhalifu.
-
Kenya inazungumza na Thailand juu ya kuwarejesha raia 64 waliokwama Myanmar
Mar 03, 2025 10:57Kenya inafanya mazungumzo na Serikali ya Thailand ili kufungua tena mpaka wa nchi hiyo na Myanmar, ikitaka kuwahamisha raia 64 wa Kenya waliookolewa hivi karibuni kutoka kwenye mitandao ya magendo ya binadamu nchini Myanmar.
-
Jordan yapinga juhudi za RSF za kuunda serikali nyingine nchini Sudan
Mar 03, 2025 10:16Jordan imepinga juhudi zozote zinazoweza kuhatarisha umoja wa Sudan, ikiwa ni pamoja na jitihada za kuundwa serikali nyingine ambazo zinafanywa na wapinzani wa jeshi la Sudan na imesema kuwa jambo hilo linaweza kushadidisha tu mgogoro wa Sudan.
-
Rais wa Guinea-Bissau atishia kuufukuza ujumbe wa ECOWAS
Mar 03, 2025 03:37Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embalo ametishia kuufukuza ujumbe wa kisiasa uliotumwa nchini mwake na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS).
-
Uganda yatuma wanajeshi zaidi DRC, huku mzozo ukiendelea
Mar 02, 2025 22:54Jeshi la Uganda limethibitisha kutuma wanajeshi wake katika mji mwingine kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupambana na makundi yenye silaha, huku kukiwa na hofu kuwa mzozo mkali unaoendelea DRC unaweza kuingia katika vita vikubwa.
-
Wanajeshi 11 wauliwa kaskazini mwa Niger
Mar 02, 2025 22:53Wanajeshi wasiopungua 11 wameuawa kaskazini mwa Niger na wengine kadhaa wamejeruhiwa.
-
WHO: Uganda imeripoti kifo kingine cha Ebola
Mar 02, 2025 08:56Shirika la Afya Duniani WHO likinukuu Wizara ya Afya ya Uganda limesema mgonjwa wa pili wa Ebola amefariki dunia katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
-
Misri yapinga kuundwa serikali nyingine nchini Sudan
Mar 02, 2025 08:54Misri imetangaza leo Jumapili kuwa haiafiki jaribio lolote la kuunda serikali nyingine nchini Sudan au kuchukuliwa hatua yoyote ambayo inatishia umoja na mamlaka ya kujitawala Sudan.
-
Mapigano mashariki mwa DRC yazidisha mateso ya Waislamu, Swala ya Tarawih yasitishwa
Mar 02, 2025 03:59Baraza Kuu la Waislamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limeamua kusimamisha Swala ya Tarawih katika miji ya mashariki inayokaliwa na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.
-
Mapigano makali yaripotiwa kandokando ya ikulu ya rais mjini Khartoum, Sudan
Mar 02, 2025 03:45Baadhi ya vyanzo vya ndani vimeripoti kuwa Jeshi la Sudan limefanya mashambulizi makali dhidi ya ngome za wapiganaji wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) mjini Khartoum na kwamba mapigano makali yanashuhudiwa karibu na ikulu ya rais.