-
Mgogoro mashariki mwa DRC waathiri zaidi ya wanafunzi milioni 1
Feb 27, 2025 07:32Kuongezeka kwa mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo waasi wa M23 wameshadidisha mashambulizi dhidi ya vikosi vya serikali, kumesababisha shule 2,594 kufungwa.
-
Misri yapinga pendekezo la Israel la kutaka Gaza isimamiwe na Cairo
Feb 27, 2025 07:31Misri imepinga pendekezo lililotolewa na kiongozi wa upinzani wa Israel, Yair Lapid kwamba Cairo, badala ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas, iendeshe na kuusimamia kwa muda Ukanda wa Gaza; na kusisitiza kuwa mipango ya aina hiyo "haikubaliki."
-
Wasomali 4.4 wanaweza kukabiliwa na njaa kufikia Aprili 2025
Feb 27, 2025 04:31Serikali ya Somalia na mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yalionya Jumatano kuwa watu milioni 4.4 wanaweza kukabiliwa na njaa kufikia Aprili 2025 kutokana na ukame unaozidi, mizozo na ongezeko la bei za chakula katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
Ugonjwa usiojulikana waua makumi nchini DRC
Feb 27, 2025 04:24Watu wasiopungua 53 wamefariki kutokana na ugonjwa usiojulikana katika wiki za hivi karibuni katika sehemu ya kaskazini-magharibi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Bunge la Algeria lakata uhusiano na Seneti ya Ufaransa kutokana na Sahara Magharibi
Feb 27, 2025 04:20Baraza la Taifa la Algeria, ambalo ni baraza la juu la bunge, lilisitisha uhusiano wake na Seneti ya Ufaransa siku ya Jumatano kufuatia ziara ya spika wa seneti hiyo katika eneo la Sahara Magharibi linalozozaniwa.
-
Waislamu wa Ghana wamuenzi na kumuomboleza Sayyid Hassan Nasrullah
Feb 26, 2025 23:47Jumuiya ya Waislamu wa Ghana mjini Accra imefanya hafla ya kumbukumbu ya Sayyed Hassan Nasrallah, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon, ambaye walimtukuza kama shahidi wa Uislamu na ubinadamu.
-
Vikosi vya serikali Sudan Kusini vyashambulia kwa bomu kambi ya kiongozi wa upinzani Riek Machar
Feb 26, 2025 23:46Hali ya wasiwasi inaongezeka tena nchini Sudan Kusini licha ya wito wa kuheshimiwa makubaliano ya amani.
-
Somalia na Umoja wa Afrika wakubaliana kuhusu wanajeshi watakaojumuishwa katika kikosi kipya
Feb 26, 2025 23:45Serikali kuu ya Somalia na Umoja wa Afrika wamekubaliana kuhusu idadi ya wanajeshi kutoka nchi mbalimbali watakaohudumu katika kikosi kipya cha Umoja wa Afrika.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda: 'Umoja wa Mataifa sio Biblia', tutaendelea kuzipinga ripoti zake
Feb 26, 2025 09:28Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe amesema, Umoja wa Mataifa sio Biblia, na kwamba nchi yake itapinga ripoti zake za madai kwamba Kigali inawaunga mkono waasi wa M23 wanaopigana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mashariki mwa nchi hiyo.
-
Operesheni ya Jeshi la Somalia yaua magaidi 70 wa Al-Shabaab katika jimbo la Hirshabelle
Feb 26, 2025 08:12Wizara ya Habari ya Somalia imetangaza kuwa vikosi vya jeshi vikishirikiana na vikosi vingine vya ndani vimewaua wanamgambo wapatao 70 wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab katika operesheni ya mashambulizi viliyotekeleza jana Jumanne katika maeneo kadhaa ya jimbo la Hirshabelle kusini mwa katikati ya nchi hiyo.