-
Gachagua amuomba Raila kuungana na wapinzani wa Rais Ruto, amuahidi urais wa Kenya mwaka 2027
Feb 26, 2025 02:39Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, amesema kwamba anaweza kumfanya kiongozi wa ODM, Raila Odinga kuwa rais wa Kenya iwapo atakubali kuungana naye na vigogo wengine wa upinzani.
-
DRC Yasitisha Usafirishaji wa Kobalti kwa Miezi Minne
Feb 25, 2025 22:51Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imesitisha usafirishaji wa kobalti kwa miezi minne ili kudhibiti usambazaji wa kobalti kwenye soko la kimataifa, ambalo kwa sasa linakabiliwa na upitilivu wa bidhaa hiyo. Hali hii imesababisha kushuka kwa bei kwa mfululizo.
-
Uwezekano wa kutokea vita katika eneo la Maziwa Makuu
Feb 25, 2025 10:21Huku vikosi vya waasi wa M23 vikiendelea kusonga mbele katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kumeongeza hatari ya kutokea vita vya pande zote katika eneo la Maziwa Makuu Afrika.
-
EAC na SADC zawateua marais wastaafu wa Afrika kusuluhisha mzozo wa Kongo DR
Feb 25, 2025 06:15Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC zimewateua Uhuru Kenyatta kutoka Kenya, Olusegun Obasanjo kutoka Nigeria, na Hailemariam Desalegn kutoka Ethiopia kuongoza mazungumzo ya kutatua mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
-
Sudan yatishia kulipiza kisasi dhidi ya Kenya kwa kuwa mwenyeji wa RSF
Feb 25, 2025 02:30Serikali ya Sudan jana Jumatatu iliapa kuchukua hatua kali dhidi ya Kenya kutokana na Nairobi kuwa mwenyeji wa kikao cha wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
-
Viongozi wa Libya na Somalia wajadiliana ushirikiano katika uwekezaji na elimu
Feb 25, 2025 02:28Mkuu wa Baraza la Uongozi la Libya, Mohamed Menfi, amesisitizia umuhimu wa kuweko ushirikiano baina ya nchi yake na Somalia katika nyuga tofauti. Mwito huo aliutoa jana Jumatatu katika mazungumzo ya pamoja na waandishi wa habari baina yake na Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliyeko ziarani nchini Libya.
-
Hujuma za waasi mashariki mwa Kongo zimeuwa watu 7,000 mwaka huu
Feb 24, 2025 23:00Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa watu zaidi ya elfu saba wameuawa mwaka huu wakati waasi wa kundi la M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wakiteka miji kadhaa katika eneo lenye utajiri wa madini mashariki mwa Kongo.
-
Senegal yasaini makubaliano ya amani na kundi linalopigania kujitenga eneo la Casamance
Feb 24, 2025 22:55Serikali ya Senegal na harakati kwa jina la Movement of Democratic Forces of Casamance (MFDC); kundi la waasi linalopigania kujitenga eneo la kusini mwa Senegal la Casamance wametia saini makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo, na hivyo kumaliza moja ya migogoro mikongwe zaidi barani Afrika, ambayo imedumu kwa miongo minne.
-
Waasi wa DRC watangaza kuwa tayari kwa usitishaji mapigano
Feb 24, 2025 08:53Muungano wa waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Alliance Fleuve Congo (AFC), unaojumuisha waasi wa M23, umetangaza kuwa tayari kushiriki mazungumzo na serikali ili kusitisha mara moja mapigano mashariki mwa nchi, msemaji wa kundi hilo amesema.
-
Jeshi la Sudan lakomboa mji mpya, latangaza mafanikio dhidi ya waasi wa RSF
Feb 24, 2025 08:52Jeshi la Sudan limekomboa mji mwingine kusini mwa Sudan siku ya Jumapili, ikiwa ni mafanikio mapya katika mapambano dhidi ya kundi la waasi wa kundi la RSF.