Waislamu wa Ghana wamuenzi na kumuomboleza Sayyid Hassan Nasrullah
Jumuiya ya Waislamu wa Ghana mjini Accra imefanya hafla ya kumbukumbu ya Sayyed Hassan Nasrallah, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon, ambaye walimtukuza kama shahidi wa Uislamu na ubinadamu.
Bw. Munir Mustapha, shakhsia mashuhuri katika jamii ya Kiislamu ya Ghana, alimuelezea Sayyed Hassan Nasrullah kama nembo ya haki.
“Mtu aliyekuwa akipigania haki, nembo ya Ubinadamu, alama ya kupiga vita dhulma, kwa hiyo aliyehudhuria kumbukumbu hiyo kwa kujitambua alipaswa kuuambia ulimwengu kuwa sisi sote ni Sayyed Hassan Nasrullah.
Saeed Sandow, mchambuzi na mtaalamu wa mahusiano ya kimataifa kutoka Ghana, pia alimuelezea Sayyed Hassan Nasrallah kama nyota wa kimataifa kwa sababu ya jukumu lake katika kuanzisha na kudumisha amani, usalama, mipaka ya maeneo, na uhuru wa kisiasa nchini Lebanon.
Nchini Nigeria pia Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo katika Jimbo la Kano imewaenzi na kuwaomboleza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyed Hassan Nasrullah na Mkuu wa zamani wa Baraza la Utendaji la harakati hiyo, Sayyed Hashem Safieddine, waliouawa shahidi katika shambulio la anga la Israel huko Beirut.
Jumapili ya Februari 23 yalifanyika mjini Beirut, Lebanon mazishi ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Shahidi Sayyid Hashim Safiyyuddin, kwa kuhuhudhuriwa na zaidi ya watu milioni moja.