-
Watu 55,600 wameathiriwa na mafuriko nchini Senegal
Oct 20, 2024 07:02Serikali ya Senegal imetangaza kuwa, mafuriko katika Mto wa Senegal yameathiri familia 774 zenye karibu watu 55,600 za nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
-
Maandamano Senegal kupinga jinai za Israel huko Lebanon na Gaza
Oct 20, 2024 01:17Maandamano makubwa yamefanyika katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, siku ya Jumamosi kupinga jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na Lebanon.
-
Jeshi la Nigeria lawaangamiza magaidi 101 ndani ya wiki moja
Oct 19, 2024 07:51Jeshi la Nigeria limewaua magaidi 101 katika wiki iliyopita katika operesheni zilizowalenga magaidi wa makundi ya Boko Haram, Jimbo la Afrika Magharibi la ISIS (ISWAP) pamoja na magenge mengine ya wahalifu.
-
UNICEF: Zaidi ya watu milioni 3 wako katika hatari ya kipindupindu nchini Sudan
Oct 18, 2024 23:29Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) jana Ijumaa lilionya kuwa zaidi ya watu milioni tatu wako katika hatari ya kuugua ugonjwa wa kipindupindu nchini Sudan.
-
Vifo vya Mpox vyapindukia 1,000 huku maambukizi yakienea katika nchi 18 za Afrika
Oct 18, 2024 10:30Bara la Afrika wiki iliyopita lilisajili vifo vipya 50 vilivyosababishwa na ugonjwa wa virusi wa Mpox na hivyo kufanya idadi ya watu waliopoteza maisha kwa ugonjwa huo kufikia 1,100 tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Ripoti hii ni kwa mujibu wa takwimu mpya za Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa barani Afrika (Africa CDC).
-
Mahakama Kuu Kenya yasimamisha uamuzi wa Bunge wa kumuidhinisha Kindiki kuwa Naibu Rais
Oct 18, 2024 10:23Mahakama Kuu nchini Kenya leo imetoa amri ya muda ya kusimamisha kubadilishwa kwa Naibu Rais wa nchi hiyo, Rigathi Gachagua.
-
Afrika Kusini: Tutafuatilia faili na mauaji ya kimbari ya Israel ICJ
Oct 18, 2024 04:29Afrika Kusini imetangaza azma yake ya kufuatilia kesi ya mauaji ya halaiki iliyowasilisha dhidi ya utawala ghasibu wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) "licha ya mashinikizo kutoka kwa baadhi ya nchi ya kuitaka kuondoa kesi hiyo.
-
HRW: Wakimbizi wa Sudan hatarini kutokana na mapigano
Oct 18, 2024 04:20Mapigano kati ya vikosi vya shirikisho vya Ethiopia na wanamgambo kaskazini magharibi mwa nchi hiyo yamewaweka katika hatari kubwa wakimbizi wa vita kutoka Sudan.
-
Baraza la Seneti Kenya lamuondoa madarakani Naibu Rais Gachagua
Oct 18, 2024 00:16Baraza la Seneti nchini Kenya limeidhinisha uamuzi wa kumuondoa madarakani Naibu Rais wa nchi hiyo Rigathi Gachagua.
-
AU yakabidhi kambi 6 za kijeshi kwa vikosi vya Somalia
Oct 17, 2024 23:21Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) kimekabidhi rasmi kambi ya kijeshi ya Kuday kwa vikosi vya usalama vya Somalia, kuashiria hatua muhimu katika awamu ya tatu ya uondoaji wa wanajeshi hao wa kigeni.