-
Nigeria kuandamana leo kupinga ongezeko la gharama za maisha
Sep 30, 2024 22:48Wananchi wa Nigeria leo Jumanne wamepanga kufanya maandamano mapya kulalamikia ongezeko la gharama za maisha. Maandamano hayo yaliyopewa jina la "Oktoba Mosi Bila Hofu" yamepangwa kwenda sambamba na kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 64 ya uhuru wa Nigeria.
-
Maelfu ya Wakenya wamekwama Lebanon huku Israel ikiendeleza mashambulizi ya kigaidi
Sep 30, 2024 04:35Maelfu ya Wakenya wamekwama nchini Lebanon huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukiendeleza mashambulizi yake ya kigaidi dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.
-
WHO kuisaidia Rwanda kukabiliana na mripuko wa kwanza wa Marburg
Sep 29, 2024 22:55Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitaka jamii ya kimataifa ishirikiane na Rwanda katika kupambana na mripuko wa kwanza wa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Marburg (MVD).
-
Pretoria: Tunatiwa wasi wasi na mauaji ya kigaidi ya Israel
Sep 29, 2024 10:45Afrika Kusini imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja nchini Lebanon, ambapo utawala wa Kizayuni wa Israel ulianza mashambulio ya anga hivi karibuni, na kuua mamia ya raia huku maelfu ya wengine wakilazimika kuyahama makazi yao.
-
Zaidi ya watu milioni 82 wanateseka kwa uhaba wa chakula Mashariki na katikati mwa Afrika
Sep 29, 2024 02:39Idadi ya watu wasio na uhakika wa chakula katika maeneo ya mashariki na katikati mwa Afrika imeshapindukia milioni 82.2. Hayo ni kwa mujibu ripoti ya Shiŕika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali ya ukanda huo.
-
Watu 17 wauawa kwa kupigwa risasi kwa umati nchini Afrika Kusini
Sep 29, 2024 02:38Polisi wa Afrika Kusini wameanzisha msako wa dharura baada ya watu 17 kupigwa risasi na kuuawa kwa umati katika mkoa wa Cape Mashariki.
-
Somalia yakumbwa na mlipuko karibu na ikulu ya Rais, watu kadhaa wauawa
Sep 28, 2024 22:47Watu kadhaa wanahofiwa kuuawa au kujeruhiwa baada ya mlipuko mkubwa kutokea leo katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
-
Human Rights Watch: Rwanda na waasi wa M23 wanashambulia raia wa Kongo DR
Sep 28, 2024 06:37Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limelituhumu jeshi la Rwanda na kundi la waasi la M23 kwamba yanafanya mashambulizi dhidi ya raia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
-
Kassim Majaliwa: Lugha ya Kiswahili iwe lugha rasmi ya 7 ya UN
Sep 28, 2024 04:00Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania amehutubia kwa mara ya kwanza Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani akimwakilisha Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
-
Mapigano yaanza tena Khartoum na El Fasher, mawasiliano yakatwa huko Omdurman
Sep 27, 2024 22:49Ripoti kutoka Sudan zinasema kuwa mapigano yamepamba moto tena kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka huko Khartoum tangu pamema jana Ijumaa.