-
Afrika Kusini yabaini maambukizi ya virusi vya Hanter vinavyohusishwa na meli ya utalii
May 06, 2026 10:24Afrika Kusini imebaini virusi kwa jina la Hanter aina ya Andes ambavyo hueneza maambukizi kutoka kwa binadamu kwenda kwa binadamu katika watu wawili waliotoka kwenye meli iliyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo. Haya yameelezwa leo bungeni na Waziri wa Afya wa nchi hiyo.
-
Marekani yatuhumiwa kulazimisha makubaliano ya afya na mikataba ya madini nchini Zambia
May 06, 2026 08:04Zambia imeishutumu Marekani kwa jaribio la kuhusisha makubaliano ya ufadhili wa sekta ya afya na mikataba ya uchimbaji madini yake ya kimkakati. Hayo yamebainika baada ya balozi wa Marekani anayemaliza muda wake kuikosoa serikali ya Zambia kwa madai ya ufisadi, udhaifu wa utawala, na ukosefu wa ushirikiano na programu za misaada ya Marekani.
-
Sudan yazituhumu Imarati na Ethiopia kushambulia uwanja wa ndege wa Khartoum
May 05, 2026 11:41Sudan leo Jumanne imrudisha nyumbani balozi wake nchini Ethiopia kwa mashauriano na kuzituhutumu Ethiopia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuwa zimehusika na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (droni) katika uwanja wa ndege wa Khartoum.
-
Kiongozi wa kijeshi Mali achukua nafasi ya waziri wa ulinzi aliyeuawa
May 05, 2026 11:25Kiongozi wa kijeshi wa Mali, Assimi Goita, atachukua wadhifa mwingine wa Waziri wa Ulinzi, kwa mujibu wa dikrii iliyotangazwa kufuatia kuuawa waziri wa wizara hiyo katika mashambulizi makubwa ya hivi karibuni nchini humo.
-
Polisi Kenya yathibitisha vifo vya watu 18 katika maporomoko ya ardhi
May 04, 2026 10:21Huduma ya Polisi ya Kenya Jumapili ilithibitisha kupoteza maisha watu 18 kufuatia maporomoko ya udongo na mafuriko huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo, na kulazimisha familia nyingi kuhama makazi yao.
-
Baada ya Ghana, Nigeria pia yamwita balozi wa Afrika Kusini kuhusu mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni
May 03, 2026 10:12Wimbi jipya la mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni, linalowalenga wahamiaji wa Kiafrika na biashara zao huko Afrika Kusini linatishia kuteteresha uhusiano wa nchi hiyo na nchi nyingine za Afrika.
-
WHO: Chanjo ya Malaria yaonyesha matumaini kwa watoto wa Cameroon
May 03, 2026 09:59Baadhi ya akina mama nchini Cameroon wamesema kuwa wameshuhudia maboresho makubwa katika afya za watoto wao baada ya kutolewa chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa malaria.
-
Rais wa zamani wa Kongo DR alaani vikwazo vya Marekani, asema si halali
May 02, 2026 09:27Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila, amelaani vikwazo vya Marekani dhidi yake kwa madai ya kuwaunga mkono waasi wa AFC/M23 mashariki mwa Kongo na kuvitaja kuwa "visivyo halali na vya matashi ya kisiasa."
-
Jeshi la Mali lakomboa mji wa mpakani baada ya shambulio la ISIS karibu na Niger
May 02, 2026 07:21Vikosi vya jeshi la Mali vimedhibiti tena mji wa karibu na mpaka wa nchi hiyo na Niger baada ya wanamgambo wanaohusishwa na ISIS kuondoka katika eneo hilo kufuatia mapigano makali, wakati jeshi likiimarisha doria kwenye maeneo hayo.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan: Tumekataa majaribio ya kulazimisha masuluhisho kutoka nje
May 02, 2026 06:59Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Mohi El-Din Salem, amefichua kwamba serikali ya nchi yake itafanya tathmini ya uhusiano wake wa kimataifa na kikanda baada ya vita, na hautakuwa sawa na hapo awali. Amesema kuwa wizara yake imezuia majaribio ya kulazimisha masuluhisho ya kigeni kwa nchi yake na haitakubali mashinikizo ya aina yoyote.