WHO: Chanjo ya Malaria yaonyesha matumaini kwa watoto wa Cameroon
-
Mafanikio ya chanjo ya kupambana na Malaria nchii Cameroon
Baadhi ya akina mama nchini Cameroon wamesema kuwa wameshuhudia maboresho makubwa katika afya za watoto wao baada ya kutolewa chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa malaria.
Katika Hospitali ya Wilaya ya Soa, akina mama wamesema kuwa ni idadi ndogo ya watoto waliopata chanjo ambao wameugua malaria.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), karibu 70% ya vifo vya malaria nchini Cameroon hutokea kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.
Chanjo hiyo, iliyosubiriwa kwa muda mrefu barani Afrika, imeonekana kuwa na ufanisi inapotolewa kwa wakati mwafaka.
Katika mahojiano na shirika la habari la Associated Press, Dk. Sania Nishtar, Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Chanjo (Gavi) amepongeza matokeo chanya ya chanjo hiyo ya kukabiliana na ugonjwa wa malaria.
"Wakati chanjo hii inatumiwa pamoja na matibabu mengine tuliyonayo; na tunapoitumia kwa wakati mwafaka kabla ya msimu wa mvua na kwa kutolewa dozi kamili, vyote husababisha kupungua vifo vya watoto, na kesi za ugonjwa zimepungua kwa asilimia 70", amesema Dakta Nishtar.