-
Rais wa Senegal avunja bunge, aitisha uchaguzi wa mapema Novemba
Sep 13, 2024 08:12Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye amelivunja bunge la nchi hiyo linaloongozwa na upinzani na kuitisha uchaguzi wa mapema ili kumaliza mvutano kati ya bunge na serikali.
-
UN: Mvua kubwa na mafuriko vinakwamisha misafara ya misaada huko Sudan
Sep 13, 2024 04:02Umoja wa Mataifa umeonya kuwa mvua kubwa na mafuriko vinatatiza usafirishaji wa misaada katika nchi za Sudan, Chad na Sudan Kusini. Taarifa hii imetolewa wakati hali ya kibinadamu katika nchi ya Sudan iliyokumbwa na vita inazidi kuwa mbaya, huku zaidi ya nusu ya wakazi wa nchi hiyo wakisumbuliwa na njaa.
-
Mwanasheria Mkuu wa Sudan: Kamati ya kutafuta ukweli ya UN ina malengo ya kisiasa
Sep 13, 2024 00:45Mwanasheria Mkuu wa Sudan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kuchunguza Uhalifu na Ukiukaji wa Sheria za Kitaifa, Kimataifa na Kibinadamu, Al-Fatih Muhammad Issa Tayfour, amesema kuwa serikali ya Khartoum na nchi zingine 16, tangu mwanzo zilikataa uamuzi wa kuunda kamati ya Umoja wa Mataifa ya kutafuta ukweli kuhusu Sudan.
-
Rais wa Guinea-Bissau: Mke wangu ameniasa nisigombee muhula wa pili
Sep 12, 2024 23:35Katika hatua ambayo imewashangaza wengi, Rais wa Guinea-Bissau Umaro Cissoko Embalo alisema jana Alkhamisi kwamba hatawania muhula wa pili katika uchaguzi wa rais unaotazamiwa kufanyika Novemba.
-
Rais wa Senegal aapa kukabiliana na magendo ya binadamu
Sep 12, 2024 23:35Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye amesema kuwa serikali yake itafanya kila liwezekanalo kukabiliana na safari hatarishi za wahamiaji baada ya mkasa wa karibuni kuua makumi ya watu.
-
Mali yaendelea 'kuviadhibu' vyombo vya habari vya Ufaransa
Sep 12, 2024 08:07Serikali ya kijeshi ya Mali imepiga marufuku kanali nyingine ya televisheni ya Ufaransa kurusha matangazo yake kwa kukiuka Sheria ya Kudhibiti Vyombo vya Habari katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
-
Umoja wa Mataifa warefusha vikwazo dhidi ya Sudan kwa mwaka mmoja mwingine
Sep 12, 2024 04:08Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limerefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Sudan kwa mwaka mmoja mwingine hadi Septemba 12, 2025.
-
Ofisi ya Rais Afrika Kusini: Tutafuatilia mashtaka yetu dhidi ya mauaji ya kimbari ya Israel
Sep 11, 2024 22:59Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini imetangaza katika taarifa yake kwamba, itaendelea kufuatilia kesi ya mauaji ya halaiki ya utawala wa Kizayuni katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) hadi hukumu yake itakapotolewa.
-
DRC yapokea dozi 50,000 za chanjo dhidi ya Mpox
Sep 11, 2024 22:59Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa, dozi 50,000 za chanjo dhidi ya Mpox ziliwasili Jumanne ya juzi, wiki moja baada ya shehena ya kwanza kutoka Umoja wa Ulaya kuwasili nchini humo.
-
Miili 26 yapatikana baada ya boti ya wahamiaji kupinduka Senegal
Sep 11, 2024 08:54Idadi ya vifo kutokana na boti iliyokuwa imebeba wahamiaji iliyopinduka katika ufuo wa Senegal imeongezeka hadi 26 kufuatia kugunduliwa kwa miili 17 zaidi Jumanne.