-
Uwanja wa ndege wa Nairobi wafungwa kufuatia mgomo wa kupinga kampuni ya India
Sep 11, 2024 08:52Uwanja wa ndege mkubwa zaidi nchini Kenya umefungwa leo Jumatano kutokana na mgomo wa wafanyikazi wakipinga pendekezo la usimamizi wa uwanja huo kukabidhiwa shirika moja la India. Mgomo huo umesababisha ucheleweshaji mkubwa na usumbufu katika safari za ndege.
-
Mashinikizo ya Israel ya kutaka Afrika Kusini isimamishe mashtaka dhidi yake huko Hague
Sep 11, 2024 03:05Utawala wa Kizayuni unalishinikiza Bunge la Marekani Congress, liizuie Afrika Kusini kuendelea na mashtaka dhidi yake Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki.
-
Wakulima wa Afrika Kusini watuhumiwa kuuwa wanawake 2, na kisha miili yao kuwalisha nguruwe
Sep 10, 2024 23:42Wanaume watatu nchini Afrika Kusini wanatuhumiwa kuwauwa wanawake wawili na kisha miili yao kuwalisha nguruwe katika shamba lao. Kesi hii tajwa imeibua ghadhabu na hasira miongoni mwa jamii ya Afrika Kusini.
-
Polisi ya Guinea-Bissau yanasa karibu tani tatu za kokeini kwenye ndege iliyotokea Venezuela
Sep 10, 2024 22:51Polisi nchini Guinea-Bissau wamenasa tani 2.6 za kokeini kutoka kwenye ndege iliyowasili katika mji mkuu wa nchi hiyo Bissau ikitokea Venezuela. Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu na Polisi ya kitengo cha vyombo vya mahakama.
-
Ethiopia yawasamehe wanajeshi 178 waliohukumiwa kifo kwa uhalifu wakati wa vita vya Tigray
Sep 10, 2024 07:46Wizara ya Ulinzi ya Ethiopia imetangaza leo Jumanne kuwa imewasamehe wanajeshi 178 waliohukumiwa kifo kwa kuhusika katika uhalifu uliotendwa wakati wa vita vya Tigray.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Misri na Sudan wakutana kujadili vita vya Sudan
Sep 10, 2024 07:44Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Badr Abdelatty, amekutana na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Sudan, Hussein Awad, na kujadiliana naye juhudi za kutatua mgogoro wa nchi hiyo.
-
Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko nchini Morocco imeongezeka hadi 18
Sep 10, 2024 03:40Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa kusini mashariki mwa Morocco imeongezeka na kufikia watu 18.
-
Somalia yafanya mkutano wa usalama na wa hali ya hewa mjini Mogadishu
Sep 09, 2024 22:57Somalia jana Jumatatu ilifanya Kongamano muhimu la Usalama na Hali ya Hewa katika mji mkuu Mogadishu, ukiwa ni mkutano muhimu wa mabadiliko ya hali ya hewa na kulinda usalama wa taifa.
-
Mashambulizi ya makombora ya wanamgambo wa RSF yaua takriban raia 21 katikati mwa Sudan
Sep 09, 2024 07:07Raia wasiopungua 21 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya wanamgambo wa kikosi cha radiamali ya haraka (RSF) kuvurumisha makombora sokoni katika mji wa Sinnar katikati mwa Sudan.
-
Makumi waaga dunia katika mripuko wa lori la mafuta nchini Nigeria
Sep 09, 2024 06:26Makumi ya watu wamepoteza maisha baada ya lori la kubeba mafuta kuripuka baada ya kugongana na gari jingine kaskazini mwa Nigeria.