-
Uganda yaripoti maambuziko mengine ya homa ya Mpox
Aug 25, 2024 03:45Wizara ya Afya ya Uganda imetangaza kuwa, visa vingine viwili vya virusi vya homa ya Mpox vimethibitishwa nchini humo na kuongeza idadi ya walioambukizwa kuwa watu wanne, katika taifa hilo la Afrika Mashariki.
-
Al-Burhan akosoa mazungumzo ya Geneva, asema kuna "njama ya kimataifa" dhidi ya Sudan
Aug 25, 2024 00:55Mkuu wa Baraza la Utawala wa Mpito na Kamanda wa Jeshi la Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan, amesema kuwa mazungumzo ya Geneva yanalenga kusafisha sura mbaya ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na wafuasi wa kundi hilo linalopigana na jeshi la Sudan.
-
Wanafunzi wa vyuo vikuu waliokuwa wametekwa nyara Nigeria waachiliwa huru
Aug 25, 2024 00:23Polisi nchini Nigeria wametangaza kuachiliwa huru wanafunzi 20 wa taaluma ya tiba waliotekwa nyara Agosti 15 katika jimbo la kati la Benue.
-
Wazairi wa Utalii na Wanyamapori Kenya: Kula nyama ya pori kunaweza kusababisha Mpox
Aug 24, 2024 23:59Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Rebecca Miano, ametoa wito kwa watu kuepuka kushika au kula nyama ya wanyamapori kutokana na tishio la ugonjwa wa Mpox.
-
UN: Mripuko mpya wa Kipindupindu Sudan unahatarisha maisha ya mamia ya maelfu ya wakimbizi
Aug 24, 2024 06:24Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limeeleza kupitia mwakilishi wake nchini Sudan Kristine Hambrouck kwamba mripuko mpya wa kipindupindu nchini Sudan, ambao ni wimbi la pili tangu vilipoanza vita miezi kumi na sita iliyopita, unahatarisha maisha ya jamii zilizolazimika kuyahama makazi yao nchini kote.
-
Almasi kubwa zaidi katika karne yapatikana nchini Botswana
Aug 24, 2024 03:13Almasi kubwa zaidi iliyowahi kupatikana katika zaidi ya karne moja imechimbuliwa katika mgodi mmoja nchini Botswana, na rais wa nchi hiyo aliuonyesha ulimwengu jiwe hilo lenye ukubwa wa ngumi katika hafla ya kulitazama.
-
Zaidi ya watu milioni 25 wamekimbia makazi yao katika Pembe ya Afrika
Aug 23, 2024 23:04Takriban watu milioni 25 walikuwa wakimbizi wa ndani katika eneo la Pembe ya Afrika mwishoni mwa Juni, ikiwa ni pamoja na wakimbizi milioni 20 wa ndani katika nchi sita na wakimbizi milioni 5 waliokimbilia nje ya nchi hizo.
-
Msumbiji yazindua mpango wa indhari ya mapema kuhusu majanga
Aug 23, 2024 06:49Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, amezindua mpango wa kitaifa wa kuhakikisha kila mtu anapata Maonyo ya Mapema kuhusu hali ya hewa, EW4All ifikapo mwishoni mwa mwaka 2027.
-
Wakuu wa masuala ya usalama wa Ethiopia na Kenya wajadili mapambano ya pamoja dhidi ya ugaidi
Aug 23, 2024 03:04Maafisa wakuu wa masuala ya kiusalama wa Ethiopia na Kenya wamesisitizia haja ya kushirikiana zaidi na kufanya kazi kwa pamoja katika kukabiliana na ugaidi.
-
Watu 26 wateketea kwa moto katika ajali mbaya ya barabarani nchini Malawi
Aug 23, 2024 03:04Takriban watu 26 wameteketea kwa moto hadi kufa nchini Malawi kufuatia kuwaka moto gari moja dogo baada ya kugonga lori la mafuta.