-
Watu milioni 63 hawana chakula cha uhakika Pembe ya Afrika
Aug 23, 2024 03:01Takriban watu milioni 63 katika eneo la Pembe ya Afrika wana uhaba mkubwa wa chakula huku watoto milioni 11 wakiwa na utapiamlo na wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.
-
Somalia kusimamisha safari za shirika la ndege la Ethiopia
Aug 22, 2024 23:26Mamlaka ya usafiri wa anga nchini Somalia imetishia kusitisha safari zote za ndege za Shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopia Airlines) kwenda nchini humo, hatua ambayo itazidi kuzorotesha uhusiano dhaifu kati ya nchi hizo jirani.
-
Utapiamlo wa watoto wafikia kiwango cha juu zaidi nchini Mali
Aug 22, 2024 23:25Nchini Mali, shirika lisilo la kiserikali la Action Against Hunger linabainisha ongezeko la kutisha la visa vya utapiamlo wa watoto katika ripoti iliyochapishwa hivi karibuni. Watoto walio na umri wa chini ya miaka 5 wanaoishi ndani ya kambi za wakimbizi kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo wameathirika zaidi.
-
Malori ya misaada yawasili Sudan baada ya kukwama kwa miezi kadhaa
Aug 22, 2024 08:31Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa zaidi ya malori 12 kutoka mashirika ya misaada yamevuka mpaka na kuingia Sudan kupitia kivuko cha Adre katika mpaka na Chad ili kuleta misaada kwa ajili ya raia walioathiriwa na njaa katika jimbo la Darfur.
-
Jeshi la Sudan: Vikosi vya Msaada wa Haraka vimepata hasara kubwa kusini mwa Khartoum
Aug 22, 2024 03:03Jeshi la Sudan limesema kuwa vikosi vya Jeshi la nchi hiyo vilifanya shambulio kubwa jana Jumatano, katika mhimili wa kitongoji cha Doha eneo la Jabra, kusini mwa Khartoum na kusababisha hasara kubwa dhidi ya wapiganaji wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).
-
Odinga aachana na siasa za Kenya, sasa anataka nafasi ya uongozi AU
Aug 22, 2024 02:35Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Bw Raila Odinga, jana Jumatano, alitangaza kwamba amejiondoa kwenye siasa za Kenya na kuingia katika siasa za Bara la Afrika katika juhudi zake za kuwania uenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika (AUC).
-
Imam wa Ghana: Arubaini ni nembo ya haki na kupinga dhulma
Aug 21, 2024 08:23Msomi mmoja mashuhuri wa Kiislamu nchini Ghana amesema matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS katika mji mtukufu wa Karbala nchini Iraq ni nembo ya mapambano ya haki na kusimama kidete dhidi ya dhulma na maonevu.
-
Watu 100 wahofiwa kufa maji katika ajali ya boti Kongo DR
Aug 21, 2024 08:22Watu zaidi ya 100 wametoweka baada ya boti iliyokuwa imewabeba kupinduka na kuzama magharibi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Wito wa kimataifa wa kutekeleza "Azimio la Jeddah" kuhusu Sudan
Aug 21, 2024 03:45Washirika wa kimataifa katika mazungumzo ya Geneva wametoa wito kwa pande zote mbili za vita nchini Sudan kutekeleza ahadi zilizotolewa katika Azimio la Jeddah zaidi ya miezi 3 iliyopita.
-
Burkina Faso, Mali, Niger zaishutumu Ukraine kwa kuunga mkono ugaidi Sahel
Aug 21, 2024 03:19Burkina Faso, Mali na Niger zimewasilisha ombi kwa Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili lilaani waziwazi kitendo cha Ukraine cha kuunga mkono ugaidi wa kimataifa" hasa katika eneo la Sahel Afrika.