Msumbiji yazindua mpango wa indhari ya mapema kuhusu majanga
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i115548-msumbiji_yazindua_mpango_wa_indhari_ya_mapema_kuhusu_majanga
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, amezindua mpango wa kitaifa wa kuhakikisha kila mtu anapata Maonyo ya Mapema kuhusu hali ya hewa, EW4All ifikapo mwishoni mwa mwaka 2027.
(last modified 2024-08-23T06:49:07+00:00 )
Aug 23, 2024 06:49 UTC
  • Msumbiji yazindua mpango wa indhari ya mapema kuhusu majanga

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, amezindua mpango wa kitaifa wa kuhakikisha kila mtu anapata Maonyo ya Mapema kuhusu hali ya hewa, EW4All ifikapo mwishoni mwa mwaka 2027.

Aidha nchi hiyo ya kusini mwa Afrika imetangaza uwekezaji mpya muhimu ili kuboresha uchunguzi wa kimsingi wa hali ya hewa. Uzinduzi uliofanyika Alhamisi  katika hafla ya ngazi ya mawaziri iliyofanyika katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo.

Ikiwa katika pwani ya kusini mashariki mwa Afrika, Msumbiji hukumbwa mara kwa mara na vimbunga vya kitropiki ambavyo hupitia Bahari ya Hindi na kusababisha mafuriko katikak maeneo mengi ya nchi hiyo inayopakana na Tanzania. Zaidi ya 60% ya watu wanaishi katika maeneo ya mwambao  na kilimo chao hutegemea mvua. Kwa msingi huo kuongeza vimbunga huharibu  miundombinu na pato la Maisha.

Mpango huo uliozinduliwa na Rais Nyusi unajumuisha mnyororo mzima wa utabiri wa hali ya hewa, kuanzia kukusanya takwimu za hali ya hewa, tabianchi, kuimarisha utabiri wa hali ya hewa, na mfumo wa utoaji wa maonyo hadi kutoa taarifa kuhusu mipango bora ya kuhimili mabadiliko tabianchi.

Rais Nyusi amesema Msumbiji ni nchi ambayo inakabiliwa na tishio la kudumu la majanga, hasa yale yanayosababishwa na majanga ya kiasili kama vile mafuriko, vimbunga na ukame.

Rais Nyusi amesema "mengi yanaweza kufanywa ili kupunguza kupoteza maisha ya binadamu na madhara makubwa zaidi.