-
Baraza la mawaziri la serikali ya umoja wa kitaifa ya Afrika Kusini laapishwa
Jul 04, 2024 03:33Baraza jipya la mawaziri la Afrika Kusini liliapishwa jana Jumatano, wakati huu ambapo serikali ya nchi hiyo inakabiliana na changamoto za uchumi na mabadiliko ya kijamii.
-
Wanajeshi 25 wahukumiwa kifo Kongo kwa kumkimbia adui
Jul 04, 2024 03:14Jumla ya washtakiwa 31, wakiwemo wanajeshi 27 na wake zao wanne ambao ni raia wa kawaida wamefikishwa katika mahakama ya kijeshi ya Butembo katika mkoa wa Kivu Kaskazini, karibu na mstari wa mbele wa vita kwa "kutoroka vitani na kumpa nafasi adui".
-
Rais Ruto aagiza kutazamwa upya nyongeza ya mishahara ya serikali
Jul 04, 2024 03:07Mapendekezo ya nyongeza ya mishahara kwa maafisa wa Serikali na wawakilishi wa Bunge la Kenya hayatatekelezwa baada ya Rais William Ruto wa nchi hiyo kuagiza kuangaliwa upya kwa mipango hiyo kufuatia malalamiko ya umma.
-
Khartoum yakanusha habari ya uwezekano wa kukutana Al Burhan na Dagalo huko Kampala
Jul 03, 2024 22:54Yasser Atta, Msaidizi wa Mkuu wa Jeshi la Suudan amekanusha habari ya kuwepo mpango wa mkutano kati ya Rais wa Baraza Kuu la Utawala nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, na kiongozi kundi la waasi wa RSF Hamdan Dagalo Hemedti, akipinga ripoti zinazodai kwamba mkutano huo utafanyika hivi karibuni nchini Uganda.
-
Kiswahili Lugha Yetu; Baraza Kuu la UN latambua rasmi Siku ya Kimataifa ya Kiswahili
Jul 03, 2024 07:21Nchi Wanachama wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa zimepitisha azimio la kihistoria lililowasilishwa na Kenya na Tanzania kwa niaba ya Kundi la Afrika na kutangaza rasmi kuwa tarehe 7 Julai ni Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili.
-
Tunisia yaandaa mkutano wa kibiashara na mataifa ya Afrika ili kukuza mauzo ya nje
Jul 03, 2024 07:21Mkutano wa 3 wa Biashara kati ya Tunisia na nchi nyingine za Afrika ulioanza jana Jumanne umeendelea leo katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis, na lengo lake ni kuongeza mauzo ya bidhaa za Tunisia kwa nchi za Afrika za chini ya Jangwa la Sahara.
-
Benki ya Dunia yaidhinisha dola milioni 207.6 za kukabiliana na ukame Zambia
Jul 03, 2024 07:13Benki ya Dunia imeidhinisha msaada wa dola milioni 207.6 wa kuisaidia serikali ya Zambia kukabiliana na ukame.
-
Watu 40 wauawa katika shambulio la wabeba silaha Mali
Jul 03, 2024 03:14Makumi ya watu wameuawa katika shambulio la genge la wabeba silaha, lililolenga kijiji kimoja cha katikati mwa Mali.
-
Zambia kujinaisha matumizi ya sarafu ya dola
Jul 03, 2024 03:13Benki Kuu ya Zambia imeandaa rasimu ya kanuni mpya zinazokusudia kuzuia matumizi ya sarafu za kigeni hususan dola ya Marekani katika miamala ya biashara ya ndani ya nchi.
-
Ripoti: Kiwango cha wawekezaji wa nje barani Afrika kimeshuka
Jul 03, 2024 00:17Imeelezwa kuwa, Afrika haikuvutia sana uwekezaji wa kigeni mwaka jana (2023) na makubaliano ya kifedha yalishuka kwa asilimia 50 mpaka dola bilioni 64, kwa mujibu wa ripoti mpya.