-
Haftar akanusha kukipatia silaha kikosi cha RSF kinachopigana na serikali ya Sudan
Jun 24, 2024 00:06Serikali ya mashariki mwa Libya, ambayo haitambuliwi na jamii ya kimataifa imekanusha taarifa zinazodai kwamba, imekuwa ikiwapatia silaha wapiganaji wa RSF wanaoongozwa na Hamdan Dagalo katika vita vya ndani nchini Sudan.
-
Wanamgambo wa CODECO waua watu 23 mashariki mwa DRC
Jun 23, 2024 23:06Zaidi ya watu 23 wanaripotiwa kuuawa na waasi wa kundi la CODECO katika vijini kadhaa kwenye jimbo lenye utajiri mkubwa wa dhahabu la Ituri kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Sudan: Hatujawahi kuuomba msamaha Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati)
Jun 23, 2024 06:52Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imekanusha habari zinazodai kuwa Khartoum imeuomba radhi Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) baada ya mwakilishi wa kudumu wa Sudan katika Umoja wa Mataifa kuishutumu Imarati kwa kuvisaidia vikosi vya RSF.
-
Kampeni za Uchaguzi Mkuu zinaendelea nchini Rwanda
Jun 23, 2024 05:49Kampeni zilizoanza jana Jumamosi nchini Rwanda zinaendelea huku wagombea watatu waliopasishwa baada ya mchujo wa walijiandikisha kugombea wakizindua kampeni zao katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo.
-
Waasi wa Codeco wauwa raia zaidi ya 20 katika jimbo la Ituri, Kongo
Jun 23, 2024 04:10Waasi kwa jina la Codeco wanatuhumiwa kuua raia zaidi ya 20 katika kijiji kimoja katika jimbo tajiri kwa madini ya dhahabu la Ituri kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Mahujaji 20 wa Morocco wapoteza maisha wakati wa Hijja nchini Saudi Arabia
Jun 22, 2024 23:16Serikali ya Morocco imetangaza kuwa, mahujaji 20 kutoka nchini humo wamefariki dunia kutokana na joto kali wakati wa ibada ya Hija ya mwaka huu nchini Saudi Arabia.
-
Mbunge akamatwa kwa "uchochezi" kuhusu ajali ya ndege nchini Malawi
Jun 22, 2024 23:15Polisi nchini Malawi wamemkamata Mbunge, Kamlepo Kalua, na mwanaharakati, Bon Kalindo, kutokana na maneno waliyoandika kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na ajali ya ndege iliyotokea Juni 10 iliyoua Makamu wa Rais wa nchi hiyo Saulos Chilima na maafisa wengine wanane.
-
Rais wa Tunisia amfuta kazi waziri kwa vifo vya makumi ya Mahujaji Makka
Jun 22, 2024 07:48Rais Kais Saied wa Tunisia amempiga kalamu nyekundu Waziri wa Masuala ya Dini wa nchi hiyo, Brahim Chaibi, akimbebesha dhima ya vifo vya makumi wa raia wa nchi hiyo, waliokuwa miongoni mwa malaki ya Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Allah mjini Makka, Saudi Arabia mwaka huu.
-
Mudavadi: Kuweka kando Muswada wa Fedha ni sawa na kuangusha Serikali ya Kenya
Jun 22, 2024 03:19Kinara wa Mawaziri wa Kenya, Musalia Mudavadi, amesema Muswada wa Fedha 2024 lazima upitishwe na kutiwa saini na Rais William Ruto kuwa sheria, akisema kinyume na hivyo itakuwa ni sawa na kuangusha Serikali.
-
Kagame: Sijawahi kuweka masharti ya kukutana na Félix Tshisekedi
Jun 22, 2024 00:53Rais Paul Kagame wa Rwanda amezungumzia uhusiano uliopo kati ya nchi yake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambao umezorota katika siku za hivi karibuni kutokana na kuongezeka mivutano.