-
Wakuu wa Misri na Somalia wakutana wakati huu Ethiopia ikilalamikia kuchafuliwa usalama wake
Oct 04, 2026 10:52Rais Abdel Fattah El-Sisi wa Misri na Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia wamefanya mazungumzo ya pamoja na kukubaliana kuimarisha uratibu wa usalama na utulivu katika Pembe ya Afrika, Ghuba ya Aden, Lango-Bahari wa Bab al-Mandab na Bahari ya Sham, wakati huu ambapo Ethiopia inawashutumu majirani zake hasa Misri na Eritrea kuwa zinaharibu usalama wake wa ndani.
-
Hali yaendelea kuwa tete Ethiopia, watu kadhaa wauawa katika shambulio la watu wenye silaha
Oct 04, 2026 04:13Hali nchini Ethiopia imeendelea kuwa tete huku maafisa wa kieneo wakitangaza kuwa, watu wenye silaha wameua maafisa kadhaa wa polisi pamoja na wafanyakazi wa masuala ya usalama, kusini mwa nchi hiyo.
-
Watu 17 waaga dunia katika ajali iliyotokea barabara ya Nairobi-Mombasa
Oct 03, 2026 11:14Watu wasiopungua 17 wamefariki dunia huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya ajali iliyohusisha magari kadhaa kutokea mapema Jumamosi kwenye barabara kuu ya Nairobi-Mombasa huko nchini Kenya.
-
Eritrea yavunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Ethiopita
Oct 02, 2026 10:17Eritrea imetangaza kupitia wizara yake ya mambo ya nje kwamba inavunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Ethiopia kujibu hatua ya Ethiopia ya kuwafukuza wanadiplomasia 10 wa nchi hiyo mjini Addis Ababa.
-
Baraza la kijeshi Guinea-Bissau lazuia rais wa zamani kurejea nchini, lataja hofu ya kiusalama
Oct 02, 2026 10:07Baraza la kijeshi linaloongoza Guinea-Bissau limezuia rais wa zamani Umaro Sissoco Embalo kurejea nchini humo, likisema hakuna mazingira salama ya kuwezesha kuwasili kwake kulikokuwa kumepangwa.
-
Botswana yaadhimisha miaka 60 ya uhuru
Oct 01, 2026 12:21Botswana imeadhimisha miaka 60 ya uhuru kupitia sherehe za kitaifa zilizojumuisha maonyesho ya kitamaduni na shughuli mbalimbali za kusherehekea, zikiakisi miongo sita ya ustahimilivu na ustawi wa taifa hilo la kusini mwa Afrika.
-
Wanajeshi wazima jaribio la utekaji nyara wa wasafiri 41 kaskazini magharibi mwa Nigeria
Oct 01, 2026 03:25Jeshi la Nigeria limesema kuwa limezima jaribio la utekaji nyara wa wasafiri wasiopungua 41 kutoka Senegal baada ya kushambuliwa na watu wanaoshukiwa ni magaidi katika eneo la kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
-
Polisi Afrika Kusini wakabiliana kwa nguvu kubwa na uchimbaji haramu wa madini
Oct 01, 2026 02:44Polisi nchini Afrika Kusini wamewatia mbaroni zaidi ya washukiwa 100 wanaohusishwa na vikundi haramu vya uchimbaji madini ambavyo pia vinahusishwa na ufyatuaji risasi katika mikahawa, hivi karibuni, katika jimbo la Gauteng.
-
Ethiopia yazituhumu Eritrea, Sudan na Misri kwamba, zinawaunga mkono wanamgambo wa Tigray
Sep 30, 2026 11:46Ethiopia imezituhumu Eritrea, Sudan na Misri kuwa zinawaunga mkono wanamgambo wa Tigray, hatua ambayo Addis Ababa inaiona kuwa tishio kwa usalama na utulivu wa nchi.
-
Rais wa Afrika Kusini ataka hatua zichukuliwe kuwalinda wanawake baada ya kupatikana miili yao11 iliyotupwa
Sep 30, 2026 02:57Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema ametoa agizo la kufanyika operesheni ya kusafisha maeneo ya manispaa yenye hatari kubwa na kuchukuliwa hatua kali dhidi ya matumizi mabaya ya pombe ili kuwalinda wanawake, kufuatia mfululizo wa mauaji uliosababisha malalamiko na hasira nchi nzima.