-
Uchaguzi Mkuu unakaribia Uganda, Polisi wazuia wapinzani kufanya kampeni Arua
Nov 20, 2025 06:46Huku Uchaguzi Mkuu ukizidi kukaribia nchini Uganda, Jeshi la Polisi la nchi hiyo limekizuia chama cha upinzani cha Jukwaa la Umoja wa Kitaifa NUP kuingia katika eneo la kampeni za uchaguzi lililokuwa limepangwa kabla kwenye mji muhimu wa Arua wa kaskazini mwa Uganda jana Jumatano.
-
Wanawake wajawazito Sudan wafanya safari ngumu za kukimbia machafuko ya El-Fasher
Nov 20, 2025 06:44Nadra Mohamed Ahmed alikuwa na ujauzito wa miezi saba wakati alipokimbia machafuko na mauaji katika mji wake wa El-Fasher nchini Sudan. Baada ya kutembea kwa karibu kilomita 40 katika barabara zisizo salama na watoto wake wawili, alipata usafiri salama hadi kwenye makazi yake mapya.
-
Watu 70 hawajulikani waliko baada ya boti kuzama mkoani Kasai, DRC
Nov 20, 2025 02:39Watu wapatao 70 hawajulikani walipo baada ya boti kuzama mtoni katika Mkoa wa Kasai katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Mgogoro wa Sahel: Tishio la Kikanda au Hatari ya Kimataifa?
Nov 20, 2025 02:11Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ametahadharisha kuhusu ukuaji na upanukaji wa makundi ya kigaidi barani Afrika na kutangaza kuwa: "Hali ya usalama, hasa katika Afrika Magharibi na eneo la Sahel, inazidi kuwa mbaya siku hadi siku."
-
Afrika Kusini imejiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa G20 uliosusiwa na Marekani
Nov 19, 2025 23:49Afrika Kusini inajiadaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa G20, unaowakutanisha viongozi kutoka mataifa tajiri duniani, kujadili masuala mbalimbali yakiwemo ya kiuchumu na kisiasa. Maandalizi ya mkutano huo utakaofanyika sikuu za Jumamosi na Jumapili ijayo yamekamilika.
-
Wapalestina wa Gaza waelezea safari yao ya siri kuelekea Afrika Kusini katika njama iliyotekelezwa na Israel
Nov 19, 2025 23:27Wapalestina walioondoka Gaza hivi karibuni kupitia njia fiche ya uhamishaji inayodaiwa kuunganishwa na ofisi ya wizara ya vita ya Israel wanasema walipelekwa nje ya eneo hilo linalokumbwa na vita bila taarifa, hati, au hata kuelewa walikokuwa wanaelekezwa.
-
Maafisa wawili wa Kenya wauawa katika hujuma ya magaidi wa al-Shabaab karibu na mpaka wa Somalia
Nov 19, 2025 23:27Maafisa wawili wa Kitengo cha Ulinzi wa Mpaka cha Kenya wameuawa Jumatano baada ya gari lao kukanyaga bomu la kutegwa ardhini (IED) lililowekwa na magaidi wakufurishaji wa al-Shabaab kutoka Somalia katika barabara ya Liboi kuelekea Kulan, kaskazini mwa Kenya.
-
Eswatini ilipokea hongo ya dola milioni 5 kutoka Marekani ili kukubali wahamiaji waliotimuliwa
Nov 19, 2025 23:26Eswatini imethibitisha kupokea dola milioni 5.1 kutoka Washington kama sehemu ya makubaliano ya kupokea wahamiaji waliofukuzwa Marekani licha ya kutokuwa na uhusiano wowote na taifa hilo la kusini mwa Afrika.
-
Katibu Mkuu wa UN: Ugaidi katika eneo la Sahel ni tishio linaloongezeka
Nov 19, 2025 09:05Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewatahadharisha viongozi duniani kwamba ugaidi katika eneo la Sahel barani Afrika ni tishio linaloongezeka duniani.
-
Rais wa Nigeria athibitisha kuuawa afisa wa ngazi ya juu wa jeshi
Nov 19, 2025 08:54Rais wa Nigeria amethibitisha kuwa Brigedia jenerali Musa Uba ameuawa na kundi la kigaidi akiwa matekani. Mauaji hayo yamefanywa siku chache baada ya afisa huyo wa ngazi ya juu wa jeshi la Nigeria kutekwa nyara na wanamgambo wa kundi la ISWAP kufuatia shambulio la kuvizia kaskazini mashariki mwa Jimbo la Borno ambalo pia liliwaua wanajeshi wanne.