-
Mkutano wa ECOWAS wafanyika Abuja, Guinea-Bissau na Benin katika ajenda
Dec 14, 2025 06:08Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) umeanza rasmi Jumapili mjini Abuja, Nigeria, ukikusanya viongozi wa kikanda kujadili masuala nyeti yanayoathiri eneo la Afrika Magharibi.
-
Taasisi za Kiislamu zaonya kuhusu njama ya Marekani dhidi ya Nigeria
Dec 14, 2025 03:39Taasisi za Kiislamu nchini Nigeria zimetangaza kuwa, hatua ya tume ya kutafuta ukweli ya bunge la Marekani ya kuandaa ripoti ya upande mmoja kuhusu mizozo ya kikabila katika nchi hiyo ya Kiafrika ni ya kuzusha mifarakano.
-
UN yalaani shambulio lililoua askari 6 wa kulinda amani Sudan
Dec 13, 2025 23:06Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameeleza kusikitishwa na shambulio la ndege isiyo na rubani lililolenga kituo cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan, na kuwaua askari sita wa kulinda amani wa umoja huo.
-
Captain Ibrahim Traoré: Burkina Faso imekuwa mfano wa kuigwa na mataifa ya bara la Afrika
Dec 13, 2025 22:39Rais wa Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traoré, amepongeza mafanikio liliyopata jeshi hivi karibuni ya kukomboa maeneo kadhaa na kusisitiza kwamba, nchi hiyo sasa imekuwa kigezo na mfano kwa mataifa ya bara la Afrika.
-
Waguinea Bissau waandamana kulaani mapinduzi, viongozi wa kanda wakutana kutafuta suluhisho
Dec 13, 2025 22:37Mamia kadhaa ya watu wameingia barabarani katika mji mkuu wa Guinea-Bissau, Bissau kupinga mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliopita viongozi wa upinzani wanaoshikiliwa waachiliwe huru, huku viongozi wa kikanda wakijiandaa kukutana leo Jumapili kujadili namna ya kuupatia suluhisho mgogoro huo.
-
Serikali ya Kongo yatoa hakikisho; yasema haitasalimu amri licha ya hali ya wasiwasi mashariki mwa nchi
Dec 13, 2025 06:22Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana Ijumaa ilitoa hakikisho ikieleza kuwa jeshi la nchi hiyo halitasalimu amri" kufuatia kutekwa mji wa Uvira.
-
UN yasikitishwa na shambulio la droni lililoua zaidi ya raia 30 Sudan
Dec 13, 2025 05:23Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesikitishwa sana na shambulio la droni yaani ndege isiyo na rubani lililoua raia wasiopungua 30 katika Jimbo la Darfur Kusini, huko Sudan.
-
WFP yaamua kupunguza mgao wa chakula kwa wanaokabiliwa na njaa nchini Sudan
Dec 13, 2025 03:53Shirika la Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa (WFP) limetangaza kwamba litaanza kupunguza mgao wa chakula unaotolewa kwa watu wa Sudan wanaokabiliwa na hatari ya njaa, kutokana na ukosefu wa ufadhili.
-
Kama ishara ya mvutano na Ethiopia: Eritrea yajiondoa tena katika jumuiya ya IGAD
Dec 13, 2025 03:03Eritrea ilitangaza jana Ijumaa kwamba imejiondoa katika Jumuiya ya Maendeleo ya Serikali za nchi za Afrika Mashariki, maarufu kama IGAD, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, akielezea wasiwasi wake kuhusu mvutano kati ya Asmara na Addis Ababa.
-
Mamia ya askari wa Afrika Magharibi wanaendelea 'kusafisha' Benin
Dec 12, 2025 23:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Benin amesema wanajeshi wapatao 200 wa Afrika Magharibi, wengi wao kutoka Nigeria na Ivory Coast, wako nchini Benin kuiunga mkono serikali kufuatia mapinduzi yaliyofeli Jumapili iliyopita.