-
Mvua kubwa na radi yaua watu 14 nchini Malawi
Dec 12, 2025 23:02Radi imeua watu 14 nchini Malawi katika muda wa wiki mbili zilizopita, huku nyumba 8,000 zikiharibiwa na kubomoka katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Afrika kufuatia kushtadi mvua kubwa nchini humo.
-
RSF yatuhumiwa kuhusika na mengi ya matukio 1,300 ya ukatili wa kingono katika vita vya Sudan
Dec 12, 2025 06:44Shirika moja la kutetea haki za wanawake limesema, limerekodi matukio yapatayo 1,300 ya vitendo vya ukatili wa kingono na kijinsia vilivyofanywa katika vita vya ndani nchini Sudan huku Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF) kikishutumiwa kuhusika na akthari ya vitendo hivyo.
-
Benki Kuu ya Ufaransa yahusishwa na mauaji ya kimbari ya Watutsi ya 1994 nchini Rwanda
Dec 12, 2025 06:41Wanaharakati wa haki za kibinadamu na watafiti mbalimbali wameituhumu Benki Kuu ya Ufaransa kwamba ilihusika kwa namna moja katika matukio yaliyopelekea kutokea mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda dhidi ya jamii ya Watutsi.
-
Rais Samia apokea hati za utambulisho za balozi wa Iran nchini Tanzania
Dec 12, 2025 03:28Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, jana alipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa mabalozi wapya watano walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao, katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.
-
UN: Mapigano yanashadidi mashariki mwa DRC
Dec 12, 2025 03:26Mapigano yanayoendelea kukithiri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yamesababisha vifo vya zaidi ya raia 70, kuwafurusha makwao zaidi ya watu 200,000 na kuwakosesha maelfu ya watu msaada wa chakula.
-
Guterres atoa wito kwa Eritrea na Ethiopia kuheshimu makubaliano ya mpaka
Dec 12, 2025 03:25Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ijumaa, amezitaka Eritrea na Ethiopia kurejea kwenye dhamira ya makubaliano yaliyomaliza rasmi uhasama kati ya mataifa hayo mawili ya Pembe ya Afrika miaka 25 iliyopita, akionya kuwa mvutano unaoibuka upya unaweza kuhatarisha amani ya eneo.
-
Sudan Kusini yatuma wanajeshi kulinda eneo muhimu la mafuta la Heglig nchini Sudan
Dec 11, 2025 23:11Sudan Kusini imetuma wanajeshi wake katika nchi jirani ya Sudan kwa lengo kulinda kisima cha kimkakati cha mafuta cha Heglig karibu na mpaka. Haya yamebainishwa jana Alhamisi na Mkuu wa jeshi la nchi siku chache baada ya Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kulidhibiti eneo hilo.
-
Watoto 100 wa shule waliotekwa nyara mwezi jana Nigeria warejea makwao baada ya kuachiwa huru
Dec 11, 2025 08:38Wanafunzi 100 wa Nigeria waliotekwa nyara mwezi uliopita katika Shule ya Kikatoliki ya St. Mary’s huko Papiri katika eneo la Gongola hatimaye wamerejea nyumbani baada ya kuachiliwa mwishoni mwa juma.
-
Waasi wa M23 wadai kuuteka mji wa kiistratejia wa Uvira, mashariki mwa Kongo
Dec 11, 2025 08:28Waasi wa M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana Jumatano walitoa taarifa wakidai kuuteka mji wa kimkakati wa Uvira, ambao ni kitovu muhimu cha kibiashara karibu na mpaka wa nchi hiyo na Burundi.
-
Watu 22 wafariki, 16 wajeruhiwa baada ya majengo mawili kuporomoka katika mji wa Fes, Morocco
Dec 11, 2025 02:41Watu wapatao 22 wamefariki dunia na wengine 16 wamejeruhiwa wakati majengo mawili ya makazi ya watu yalipoporomoka katika mji wa Fes ulioko kaskazini mwa Morocco, jana Jumatano.