-
Waziri Mkuu wa zamani na mkongwe wa siasa za Kenya Raila Odinga afariki dunia akiwa matibabuni India
Oct 15, 2025 04:27Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga amefariki dunia leo asubuhi huko Koothattukulam, wilayani Ernakulam nchini India, baada ya kupata mshtuko wa moyo wakati anafanya matembezi yake ya kila asubuhi.
-
Afrika Kusini: Kesi ya mauaji ya kimbari tuliyofungua ICJ dhidi ya Israel itaendelea licha ya vita kusitishwa
Oct 15, 2025 02:32Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema usitishaji vita wa Ghaza hautaathiri kesi ya mauaji ya kimbari iliyofunguliwa na nchi yake dhidi ya utawala wa kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).
-
Mahakama ya Madagascar "yamwita" kanali wa jeshi akachukue uongozi na kuitisha uchaguzi
Oct 15, 2025 02:32Mahakama ya Juu ya Katiba ya Madagascar jana Jumanne "ilimwita" kamanda wa Kituo cha Uendeshaji cha Wafanyakazi wa Jeshi (CAPSAT) Kanali Michael Randrianirina "akatekeleze kazi za mkuu wa nchi."
-
Chama cha rais wa Gabon chapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Bunge
Oct 15, 2025 02:31Chama tawala cha Rais wa Gabon Brice Oligui Nguema, cha Muungano wa Kidemokrasia wa Wajenzi (Democratic Union of Builders) (UDB) kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Bunge, kwa kunyakua viti 102 kati ya 145 baada ya kutangazwa matokeo ya duru ya kwanza na ya pili ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika nchini humo.
-
Rajoelina atangaza kulivunja Bunge la Madagascar akiwa 'mafichoni'
Oct 14, 2025 23:04Rais wa Madagascar anayesakamwa na mashinikizo ya kujiuzulu, Andry Rajoelina ametangaza kulivunja Bunge kufuatia wiki kadhaa za maandamano dhidi ya serikali yake kote nchini, akisema ni muhimu kurejesha utulivu na kutoa nafasi kwa vijana.
-
UN: Makubaliano ya amani ya Kongo na Rwanda 'hayaheshimiwi'
Oct 14, 2025 09:17Umoja wa Mataifa umesema kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda "hayaheshimiwi."
-
Kiongozi wa upinzani Cameroon Issa Tchiroma Bakary ajitangaza mshindi wa kiti cha urais
Oct 14, 2025 09:16Issa Tchiroma Bakary kiongozi wa upinzani nchini Cameroon ametangaza kwa upande mmoja kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa juzi Jumapili akimbwaga mshindani wake mkuu Rais Paul Biya ambaye amekuwa madarakani Cameroon kwa miaka 43.
-
Mkutano wa G20 kuhusu mazingira waanza kufanyika nchini Afrika Kusini
Oct 14, 2025 02:50Mkutano wa Tatu na G20 wa mwisho wa Kikosi Kazi cha Mazingira na Ulinzi Endelevu wa Hali ya Hewa (ECSWG) ulifunguliwa rasmi jana Jumatatu mjini Cape Town, Afrika Kusini.
-
Baadhi ya ripoti: Rais wa Madagascar ametorokea Ufaransa
Oct 14, 2025 00:23Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa Rais Andry Rajoelina wa Madagascar ameikimbia nchi hiyo na kuelekea Ufaransa.
-
Jeshi la Sudan ladai kuua zaidi ya wapiganaji 100 wa RSF magharibi mwa nchi
Oct 13, 2025 22:58Jeshi la Sudan (SAF) limetoa taarifa na kudai kuwa, zaidi ya wapiganaji 100 wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) wameuawa katika mapigano ya El Fasher, makao makuu ya Jimbo la Darfur Kaskazini huko magharibi mwa Sudan.