Balozi wa Russia nchini Sudan: Mamluki wa Ukraine wanaendeshaji droni huko Darfur
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i132930-balozi_wa_russia_nchini_sudan_mamluki_wa_ukraine_wanaendeshaji_droni_huko_darfur
Balozi wa Russia nchini Sudan, Andrey Chernovol, ameripoti kwamba kuna uvumi unaosambaa nchini Sudan kuhusu uwepo wa Waukreini wanasimamia operesheni za ndege zisizo na rubani katika safu ya waasi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
(last modified 2025-11-08T07:15:37+00:00 )
Nov 08, 2025 07:15 UTC
  • Balozi wa Russia nchini Sudan: Mamluki wa Ukraine wanaendeshaji droni huko Darfur

Balozi wa Russia nchini Sudan, Andrey Chernovol, ameripoti kwamba kuna uvumi unaosambaa nchini Sudan kuhusu uwepo wa Waukreini wanasimamia operesheni za ndege zisizo na rubani katika safu ya waasi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).

Chernovol amesema katika mahojiano na shirika la habari la Novosti kwamba: "Makamanda wa RSF waliovamia mji mkuu wa Darfur Kaskazini, El Fasher, wamewapiga risasi wagonjwa hospitalini mbele ya kamera na kufanya mauaji ya halaiki dhidi ya raia, wakiwemo wanawake na watoto.

Ameongeza kuwa, walifanya kila kitu kinachoitwa 'mangamizi ya kikabila' dhidi ya jamii za Kiafrika za wenyeji. Balozi wa Russia nchini Sudan amesema: "Mamluki wa kigeni (kutoka Sudan Kusini, Chad, Colombia, na wengine) wameonekana katika matukio haya na kwa mujibu wa upande wa Sudan, sasa ndio wanaounda idadi kubwa (si chini ya 80%) ya wapiganaji wa vikundi vya waasi. Pia kuna uvumi kuhusu uwepo wa wataalamu wa ndege zisizo na rubani kutoka Ukraine."

Ni vyema kuashiria hapa kuwa shirika la habari la Novosti hapo awali lilinukuu Kitengo cha 6 cha Jeshi la Nchi kavu la Sudan kikisema kwamba mamluki wa Ukraine waliokuwa wakipigana bega kwa bega na waasi nchini Sudan wameuawa huko Darfur, na kwamba miongoni mwao walikuwamo wataalamu wa ndege zisizo na rubani.

Awali, Kanali Fath Al-Sayyed wa Shirika la Ujasusi la Jeshi la Sudan aliliambia shirika hilo kwamba mamluki kutoka Ukraine na Colombia, waliokuwa wakipigana pamoja na Vikosi vya Msaada wa Haraka nchini Sudan, waliuawa katika mapigano magharibi mwa nchi, na kwamba walikuwa wakitumia ndege zisizo na rubani zilizotengenezwa Ukraine.