-
Mashambulio ya siku tatu mtawalia ya RSF yaua watu 450 Darfur, magharibi mwa Sudan
Apr 14, 2025 06:11Harakati ya Jeshi la Ukombozi wa Sudan, inayoongozwa na Minni Arko Minnawi (SLA-Minnawi), gavana wa jimbo la Darfur magharibi mwa nchi hiyo, imetangaza kuwa watu 450 wameuawa kutokana na mashambulizi ya siku ya tatu mtawalia yaliyofanywa na wapiganaji wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) katika mji wa El Fasher, makao makuu ya eneo hilo, na kwenye kambi za wakimbizi.
-
UNICEF: Machafuko na njaa vinatishia maisha ya maelfu ya watoto wa Sudan
Mar 29, 2025 03:11Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limetangaza kuwa, ghasia na njaa vinatishia maisha ya watoto wa Sudan hususan katika mzozo wa jimbo la Darfur Kaskazini.
-
Ripoti ya UN: RSF inashambulia na kuua raia Darfur, Sudan kwa msingi wa ukabila
Mar 02, 2024 03:08Ripoti mpya ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa imesema, Vikosi vya Usaidizi wa Haraka RSF pamoja na wanamgambo vinaoshirikiana nao wanaopigania kutwaa madaraka nchini Sudan wamefanya mauaji ya kikabila na ubakaji wakati wa udhibiti wa eneo kubwa la Darfur magharibi mwa nchi hiyo, na kwamba vitendo hivyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.
-
UNHCR: Watu elfu nne wameuliwa Darfur, Sudan, mali za raia zimeharibiwa
Oct 18, 2023 03:50Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema, watu wapatao 4,000 wameuawa huku mali za raia zikiharibiwa katika mapigano yanayoendelea huko jimboni Darfur nchini Sudan, mapigano ambayo yalianzia kwenye mji mkuu Khartoum miezi sita iliyopita na kusambaa hadi nje ya mji huo, kati ya Jeshi la Serikali (SAF) na wanamgambo wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF).
-
Umoja wa Mataifa wataka kusitishwa mara moja 'mauaji ya kiholela' huko Darfur, Sudan
Jun 25, 2023 11:51Umoja wa Mataifa umetaka kusitishwa haraka iwezekanavyo mauaji ya kiholela ya raia wanaokimbia mapigano huko Darfur magharibi mwa Sudan. Umoja wa Mataifa umesema kuwa maelfu ya miili ya watu ambayo haijazikwa imesalia mitaani na ndani ya nyumba katika jimbo hilo lililoathiriwa na vita.
-
Watu 24 wauawa katika mapigano ya kikabila Darfur, Sudan
Apr 14, 2023 02:28Serikali ya Sudan imetangaza kuwa itachukua hatua kuunda jimbo jipya huko Darfur magharibi mwa nchi hiyo fikapo mwishoni mwa mwaka huu; eneo linalopakana na Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
-
Watu 200 wauawa katika jimbo la Darfur, jeshi la Sudan linatuhumiwa kuhusika
Apr 27, 2022 03:48Zaidi ya watu 200 wameuawa huko Darfur, magharibi mwa Sudan kwenye mpaka wa nchi hiyo na Chad, katika mapigano mapya ambayo yalianza hapa na pale katika eneo hilo na baadaye yakageuka kuwa mapigano makali.
-
Watu 160 wauawa katika mapigano mapya Darfur, Sudan
Apr 25, 2022 10:40Watu wasiopungua 160 wameuawa katika jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan baada ya kuibuka mapigano baina ya makundi mawili hasimu.
-
Mapigano ya kikabila Darfur yasababisha vifo vya makumi ya watu
Apr 01, 2022 10:25Mapigano makali kati ya makundi hasimu huko Darfur nchini Sudan yamesababisha takriban watu 45 kuuawa, huku viongozi wa kikabila wakiripoti kwamba mapigano hayo ni sehemu ya ghasia za kikabila zinazoendelea katika eneo hilo.
-
Watu 16 wauawa katika mapigano ya kikabila Darfur, Sudan
Mar 09, 2022 10:22Watu wasiopungua 16 wameuawa huku wengine wengi wakijeruhiwa katika mapigano ya kikabila katika mkoa wa Darfur Magharibi nchini Sudan.