-
Zarif: Marekani inahofia kushindwa katika uga wa diplomasia
Aug 10, 2019 23:31Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Marekani ina wasiwasi na kuhofia kushindwa katika uga wa diplomasia.
-
Jeshi la Iran lazindua mfumo wa rada wa Falaq wa ulinzi wa anga
Aug 10, 2019 10:59Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo limezindua mfumo wa rada wa ulinzi wa anga uliopewa jina la Falaq katika hafla iliyohudhuriwa na Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi.
-
Zarif: Iran haitasita kulinda usalama wake katika Ghuba ya Uajemi
Aug 10, 2019 02:53Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Ghuba ya Uajemi ni kipaumbele cha kwanza kwa usalama wa taifa la Iran na mesisitiza kuwa Iran haitasita katika kulinda usalama wake katika Ghuba ya Uajemi.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Iran itakabiliana na sera za kujitanua za Marekani
Aug 09, 2019 07:46Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran amesema kuwa Iran imesimama imara na kuwa macho mbele ya sera za kupenda kujitanua za Marekani na kusisitiza kuwa, Marekani imeshindwa kuyaangusha Mapinduzi ya Kiislamu na haiba na udhibiti wake umeporomoka.
-
New York Times yafichua malengo ya majasusi wa CIA kuhusu biashara na miamala ya mafuta ya Iran
Aug 09, 2019 06:19Gazeti moja la Marekani limefichua kwamba mtandao wa kijasusi ambao wanachama wake walikamatwa na Iran siku chache zilizopita ulikuwa ukifanya kazi ya kukusanya taarifa za kijasusi kuhusu biashara na miamala ya mafuta ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Usalama wa Ghuba ya Uajemi utadhaminiwa kwa ushirikiano wa majirani
Aug 09, 2019 04:59Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejadiliana, kupitia mazungumzo ya simu, na Mawaziri wenzake wa Ulinzi wa Qatar, Oman na Kuwait kuhusu umuhimu wa kudhaminiwa usalama wa Ghuba ya Uajemi kupitia ushirikiano wa pamoja.
-
Wito wa Umoja wa Mataifa kwa Marekani wa kutimiza wajibu wake wa kidiplomasia kuhusiana na Zarif
Aug 08, 2019 22:38Kuwekewa vikwazo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif na serikali ya Trump kumetafsiriwa na wengi kama ishara ya kuemewa na kuzidiwa nguvu Marekani na diplomasia imara na amilifu ya Tehran. Na kitendo hicho kimeibua hisia kali na ukosoaji mkubwa dhidi ya Washington duniani.
-
Shamkhani: Ngano ya kwamba "Israel haishindwi" imefeli
Aug 08, 2019 22:28Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa katika vita vya siku 33 vya Lebanon muqawama wa Kiislamu na harakati ya Hizbullah ya Lebanon ilifelisha ngano inayodai kwamba jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel halishindwi.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran: Marekani ndio chanzo hasa cha kukosekana amani katika eneo
Aug 08, 2019 08:01Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, muungano wa kijeshi unaotaka kuundwa na Marekani wa kisingizio cha kudhamini usalama wa vyombo vya majini ndio utakaosababisha kuvurugika zaidi amani na usalama katika eneo.
-
Sayyid Abbas Mousavi: Iran inakaribisha kwa mikono miwili ushirikiano na majirani zake
Aug 08, 2019 03:37Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inatoa kipaumbele katika siasa zake za kigeni suala la kuimarisha ushirikiano na majirani zake.