Shamkhani: Ngano ya kwamba "Israel haishindwi" imefeli
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55263-shamkhani_ngano_ya_kwamba_israel_haishindwi_imefeli
Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa katika vita vya siku 33 vya Lebanon muqawama wa Kiislamu na harakati ya Hizbullah ya Lebanon ilifelisha ngano inayodai kwamba jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel halishindwi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 09, 2019 02:58 UTC
  • Shamkhani: Ngano ya kwamba

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa katika vita vya siku 33 vya Lebanon muqawama wa Kiislamu na harakati ya Hizbullah ya Lebanon ilifelisha ngano inayodai kwamba jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel halishindwi.

Ali Shamkhani jana Alhamisi alimtumia ujumbe  Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon akimpongeza kwa maadhimisho ya ushindi wa muqawama wa Kiislamu katika vita vya siku 33 na kueleza kuwa: Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon hii leo pia umeweza kuinusuru dunia na hatari ya ugaidi wa makundi ya kitakfiri kwa kushirikiana na harakati nyingine za mapambano, kujitolea na kuwa tayari kufa shahidi. 

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameongeza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unapasa kujia kwamba, Hibullah siku zote imekuwa ikifuatilia kwa umakini mkubwa hila na chokochoko zote za utawala huo na imetoa kipigo kwa Wazayuni katika medani mbalimbali za mapambano.

Shamkhani ameashiria uaminifu, ujasiri na weledi wa Sayyid Hassan Nasrullah na mchango wake katika kuleta umoja na mshikamano ndani ya Lebanon na amani na usalama katika mipaka ya nchi hiyo na kusisitiza kwamba: Kama alivyobainisha Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, utawala wa Kizayuni hautaiona miaka 25 ijayo na karibuni hivi tutashuhudia Palestina ikikombolewa. 

Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon
 

Vita vya siku 33 kati ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel na wanamuqawama wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon vilianza mwezi Julai mwaka 2006 na kumalizika Agosti 14 mwaka huo huo kwa kupata ushindi harakati ya Hizbullah. Utawala wa Kizayuni ulilazimika kusitisha vita baada ya kupata hasara na kipigo kikali katika vita hivyo.