-
Sheikh Isa Qassim: Trump anataka kuiuza Palestina na matukufu yake
Jun 25, 2019 02:25Mwanazuoni maarufu wa Kiislamu nchini Bahrain, Sheikh Isa Qassim sambamba na kulaani hatua ya utawala wa Manama kuwa mwenyeji wa Kongamano la Kibiashara linalotazamiwa kuanza leo nchini humo kwa shabaha ya kuzindua mpango wa 'Muamala wa Karne' amesema mpango huo wa Rais Donald Trump wa Marekani unakusudia kuwapokonya Wapalestina haki zao zote na kuuza kila kitu kinachomilikiwa nao yakiwemo maeneo matakatifu.
-
Mazungumzo ya Mkuu wa Jumuiya ya Mabunge ya Dunia mjini Tehran
Jun 24, 2019 13:34"Mzizi wa matatizo mengi ya eneo la Mashariki ya Kati na dunia kwa ujumla ni udikteta wa baadhi ya nchi hususan Marekani ambayo inatekeleza sera za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja na kukiuka sheria za kimataifa."
-
Zarif: Vikwazo vya Marekani vinalemaza vita dhidi ya mihadarati
Jun 24, 2019 08:22Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema vikwazo vya upande mmoja vya Marekani na ugaidi wa kiuchumi wa nchi hiyo ya kibeberu dhidi ya taifa la Iran umekuwa kizingiti kikubwa katika ushirikiano wa kimataifa hususan katika vita dhidi ya mihadarati.
-
Iran yavunja mashambulizi milioni 33 ya kompyuta dhidi yake katika kipindi cha mwaka mmoja hasa ya Marekani
Jun 24, 2019 03:25Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema kuwa mashambulizi ya hivi karibuni ya kompyuta ya Marekani dhidi ya mfumo wa makombora wa Iran yameshindwa kuleta utata wowote na kwamba mwaka jana pekee Tehran ilifanikiwa kuvunja makumi ya mamilioni ya mashambulizi ya kompyuta dhidi yake.
-
Sanders: Trump amelazimika kuzima moto aliouwasha dhidi ya Iran
Jun 23, 2019 22:30Seneta Bernie Sanders ambaye ametangaza azma yake ya kugombea tena urais katika uchaguzi wa urais nchini Marekani mwaka ujao amesema Rais Donald Trump wa nchi hiyo amelazimika kuzima moto wa mgogoro na taharuki aliouwasha mwenyewe dhidi ya Iran.
-
Bunge la Iran launga mkono hatua ya Sepah ya kutungua drone ya Marekani
Jun 23, 2019 08:58Wabunge wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) wamelipongeza Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) kwa kutungua ndege isyo na rubani ya Marekani iliyokuwa imeingia kinyume cha sheria katika anga ya Iran.
-
Rouhani: Uingiliaji wa kijeshi wa Marekani ni chanzo cha matitzo katika eneo
Jun 23, 2019 08:42Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema sera za Iran ni kupunguza taharuki, kujiweka mbali na kila aina ya makabiliano ya kijeshi sambamba na kueneza amani na uthabiti katika eneo na dunia nzima.
-
Zarif: Iran inafanya mazungumzo na nchi mbalimbali kuhusu makubaliano ya kifedha
Jun 23, 2019 03:18Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Tehran inafanya mazungumzo na nchi mbalimbali ili kufikia makubaliano ya kifedha.
-
Majibu makali ya Tehran kwa uchokozi wa Marekani; kutekeleza jukumu la kisheria vikosi vya ulinzi vya Iran
Jun 23, 2019 02:10Taifa la Iran na vikosi vyake vya ulinzi halitaki vita, lakini daima liko imara katika kujihami na kulinda haki zake.
-
Balozi wa Imarati Tehran aitwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran
Jun 22, 2019 22:58Baada ya ndege ya Marekani kuingia katika anga ya Iran na kufanya ujasusi ikitokea katika kambi moja ya kijeshi ya Marekani huko Imarati, balozi mdogo wa Umoja wa Falme za Kiarabu hapa Tehran ameitwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ili kukabidhiwa malalamiko ya Tehran juu ya kwa nini Abu Dhabi inaruhusu ardhi yake kutumiwa kufanya ujasusi dhidi ya majirani zake.