Balozi wa Imarati Tehran aitwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i54279-balozi_wa_imarati_tehran_aitwa_wizara_ya_mambo_ya_nje_ya_iran
Baada ya ndege ya Marekani kuingia katika anga ya Iran na kufanya ujasusi ikitokea katika kambi moja ya kijeshi ya Marekani huko Imarati, balozi mdogo wa Umoja wa Falme za Kiarabu hapa Tehran ameitwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ili kukabidhiwa malalamiko ya Tehran juu ya kwa nini Abu Dhabi inaruhusu ardhi yake kutumiwa kufanya ujasusi dhidi ya majirani zake.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Jun 22, 2019 22:58 UTC
  • Balozi wa Imarati Tehran aitwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

Baada ya ndege ya Marekani kuingia katika anga ya Iran na kufanya ujasusi ikitokea katika kambi moja ya kijeshi ya Marekani huko Imarati, balozi mdogo wa Umoja wa Falme za Kiarabu hapa Tehran ameitwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ili kukabidhiwa malalamiko ya Tehran juu ya kwa nini Abu Dhabi inaruhusu ardhi yake kutumiwa kufanya ujasusi dhidi ya majirani zake.

Mkuu wa Idara ya Ghuba ya Uajemi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amemlalamikia vikali balozi mdogo wa Umoja wa Falme za Kiarabu hapa Tehran na kusisitiza kuwa, Tehran haiwezi kukubaliana na nchi yoyote inayotoa ardhi yake kutumika dhidi ya mamlaka ya kujitawala Iran majini, ardhini na angani na kwamba nchi inayofanya hivyo haiwezi kujivua na lawama katika jambo kama hilo.

Ijumaa tarehe 21 Juni 2019, balozi wa Uswisi hapa Tehran ambaye ndiye anayelinda manufaa ya Marekani nchini Iran aliitwa na Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran ili kukabidhiwa malalamiko makali ya Tehran, kufuatia ndege ya kijasusi ya Marekani kuingia katika anga ya Iran na kufanya ujasusi kabla haijatunguliwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) Alkhamisi alfajiri.

Kabla ya hapo pia, Brigedia Jenerali Hajizadeh alitoa maelezo kamili kuhusu harakati za drone hiyo ya kijasusi ya Marekani ambayo ilianza safari yake ya kijasusi saa sita na dakika 14 Alkhamisi  usiku ikitokea uwanja mmoja wa ndege za kivita wa Umoja wa Falme za Kiarabu kabla ya kutunguliwa saa 10 na dakika 5 alfajiri karibu na Kouh-e-Mobarak katika eneo la Jask mkoani Hormozgan kusini mwa Iran.