-
Duru ya nne ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja baina ya Iran na Marekani kuanza kesho
May 10, 2025 03:30Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Badr Al-Busaidi, ambaye anakaimu nafasi ya mpatanishi kati ya Iran na Marekani katika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja, ametangaza kuwa duru ya nne ya mazungumzo hayo itafanyika mjini Muscat kesho Jumapili.
-
Iran: Ripoti ya kituo cha nyuklia cha siri ni uzushi wa Netanyahu ili kuvuruga mazungumzo na Marekani
May 10, 2025 01:00Iran imekanusha ripoti kuhusu kituo cha siri cha nyuklia, ikisema zimetolewa na kundi la kigaidi la MKO kwa agizo la waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa nia ya kuvuruga mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Tehran na Washington.
-
Iran: Marekani inapotosha ukweli kuhusu urutubishaji wa urani
May 10, 2025 00:55Behrouz Kamalvandi, msemaji na naibu mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI), amepinga kauli za hivi karibuni zilizotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio kwamba ni nchi zenye silaha za nyuklia pekee zinazorutubisha madini ya urani yanayotumika kuzalisha umeme wa nyuklia.
-
Utayarifu wa Iran wa kufanya jitihada za kutatua mzozo wa India na Pakistan
May 10, 2025 00:51Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Droupadi Murmu wa India ambapo ameashiria mvutano wa hivi sasa kati ya nchi hiyo na Pakistan na kutangaza kuwa, Iran iko tayari kufanya juhudi za aina yoyote ili kusaidia jitihada za kupunguza mivutano na kuimarisha amani katika eneo hilo muhimu.
-
Ayatullah Khatami: Trump amejiongezea maadui kwa madai ya kubadilisha Ghuba ya Uajemi
May 09, 2025 07:59Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema: "Kwa kudai kubadili jina la Ghuba ya Uajemi, Trump amewageuza Wairani wote wakiwemo wanamapinduzi, wasiokuwa wapinduzi, wapinzani na wasiokuwa wapinzani, kuwa maadui zake, jambo ambalo ni ishara ya upumbavu wake."
-
Araghchi kufanya safari Saudi Arabia na Qatar kwa shughuli za kidiplomasia
May 09, 2025 07:24Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anatazamiwa kuzuru Saudi Arabia na Qatar Jumamosi ya kesho ikiwa ni sehemuu ya juhudi mpya za kuimarisha uhusiano na majirani wa eneo hili.
-
Kamanda Mkuu wa IRGC: Iran itapiga popote patakapotumika kulenga maslahi yake
May 09, 2025 04:09Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Meja Jenerali Hossein Salami amesema Iran itapiga mahala popote ambapo adui atapatumia kuishambulia nchi hii.
-
Ndege za Iran zimeimarishwa kwa makombora tuli ya masafa marefu
May 08, 2025 23:38Kamanda wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Ndege zote za kivita za Jeshi la Anga zina silaha, vifaa na makombora ya kisasa ya masafa marefu yaliyotengenezwa humu humu nchini."
-
Iran: White House haiwezi kubadilisha ukweli kuhusu Jina la Ghuba ya Uajemi
May 08, 2025 07:36Ujumbe wa Iran katika Umoja wa Mataifa umelaani vikali jaribio lolote linaloweza kufanywa na Marekani kwa ajili ya kubadilisha jina la Ghuba ya Uajemi, na kusisitiza kwamba ukweli wa kihistoria hauwezi kubadilishwa kwa maamuzi ya kisiasa.
-
Araghchi akiwa India: Iran inataka mvutano upungue kwani eneo linahitaji amani
May 08, 2025 07:31Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, amesema kuwa Tehran inazitaka India na Pakistan kujizuia na kuepusha kuongezeka kwa mvutano katika eneo hilo.