Larijani: Israel imedhoofika kutoka na wimbi la makombora ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i129656-larijani_israel_imedhoofika_kutoka_na_wimbi_la_makombora_ya_iran
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran (SNSC), Ali Larijani amesema kuwa, wimbi la mashambulio ya makombora ya Iran lilimfanya adui Mzayuni akate tamaa kikamilifu wakati wa vita vya siku 12 vya Israel ilivyoitwisha Jamhuri ya Kiislamu.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Aug 17, 2025 23:59 UTC
  • Larijani: Israel imedhoofika kutoka na wimbi la makombora ya Iran

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran (SNSC), Ali Larijani amesema kuwa, wimbi la mashambulio ya makombora ya Iran lilimfanya adui Mzayuni akate tamaa kikamilifu wakati wa vita vya siku 12 vya Israel ilivyoitwisha Jamhuri ya Kiislamu.

Akizungumza katika mahojiano kuhusiana na malengo ya safari yake ya kwanza katika nchi jirani ya Iraq akiwa Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, Dakta Larijani amesema kuwa, hakuna shaka kuwa masuala ya kieneo yamekuwa na yanasalia kuwa kipaumbele kwa maslahi ya nchi na usalama wa taifa.

Kiongozi Muahamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alimteua mwanasiasa huyo mkongwe mapema mwezi huu wa Agosti, kuwa mwakilishi wake katika Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran.

Akiashiria vita vya siku 12 vya Marekani na Israel dhidi ya nchi hii kuanzia Juni 13, afisa huyo wa ngazi ya juu wa usalama wa Iran amebainisha kuwa, utawala wa Kizayuni ulikuwa na mifumo ya kisasa zaidi ya ulinzi wa makombora, lakini misururu ya makombora ya Iran kati vita hivyo vya kichokozi iliwatia kiwewe na kuwakatisha tamaa kabisa Wazayuni.

"Wakati wa vita vya kutwishwa vya Israel dhidi ya Iran, maadui walidhani kwamba nchi za Kiislamu hazingeiunga mkono Iran kutokana na baadhi ya tofauti zao, lakini nchi hizo (za Kiislamu), serikali na wananchi wao wote, walisimama na Iran," amebainisha Larijani, ambaye ni mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Baraza Kuu la Usalama la Taifa.

Dakta Larijani ameongeza kuwa, wakati wa safari yake nchini Iraq, masuala ya usalama na kuimarisha uhusiano wa kitamaduni na kiuchumi yalijadiliwa kati ya pande hizo mbili.