-
Ebrahim Raisi: Iran yenye nguvu ina uwezo wa kuondoa chaguo la kijeshi kwenye meza ya adui
May 08, 2024 03:45Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Operesheni ya "Ahadi ya Kweli" ilileta fahari ya kitaifa na akaielezea kuwa ni dhihirisho la wazi kabisa la mantiki ya Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Iran na Oman zataka kukomeshwa haraka jinai za Israel Gaza
May 08, 2024 03:43Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Oman wametoa mwito wa kukomeshwa haraka iwezekanavyo jinai za utawala haramu wa Israel huko Gaza Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Iran yalaani mashambulizi ya Israel huko Rafah, Ukanda wa Gaza
May 07, 2024 23:46Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali mashambulizi ya utawala unaotekeleza mauaji ya kimbari wa Israel katika mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.
-
Eslami: Mienendo ya kiuhasama ya Israel isiathiri uhusiano wa Iran na IAEA
May 07, 2024 22:53Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesema hatua na mienendo ya kiuadui ya utawala wa Kizayuni wa Israel haipasi kuathiri uhusiano na ushirikiano baina ya Tehran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).
-
Hija ya kujibari na mushrikina
May 07, 2024 22:52Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, kwa kuzingatia Aya za Qur'ani Tukufu na kumbukumbu ya jina lililobarikiwa la Nabii Ibrahim (AS), ibada ya Hija ya mwaka huu inapaswa kuwa zaidi ya Hija ya kila mwaka, na inabidi iwe Hija na kutangazwa kujitenga au kujibari na adui wa Waislamu, Mzayuni mtenda uhalifu na wafuasi wake wa nchi za Marekani, Uingereza na Wamagharibi kwa ujumla.
-
Meja Jenerali Salami: Ikiwa Waislamu wataacha jihadi basi wataishi kidhalili
May 07, 2024 08:08Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (SEPAH) amesema kuwa, ubeberu unaamiliana na ulimwengu wa Kiislamu kwa sera na siasa moja na wala haujali mipaka na kusisitiza kuwa, iwapo adui atadhibiti eneo la Kiislamu basi atapanua hadi sehemu nyingine.
-
Safari ya Grossi nchini Iran na kuwekwa wazi maendeleo ya amani ya nishati ya nyuklia ya Iran
May 07, 2024 04:47Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA aliwasili mjini Tehran Jumatatu akiongoza ujumbe alioandamana nao kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa kimataifa wa nyuklia na vilevile kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa nyuklia na kisiasa wa nchini.
-
Tehran: Ushirikiano wa Iran na IAEA usiathiriwe na mwenendo usio thabiti wa US
May 07, 2024 03:55Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, kwa kutilia maanani rekodi ya Marekani ya kuhalifu ahadi katika mikataba ya huko nyuma kuhusiana na mpango wa amani wa nyuklia wa Iran, ushirikiano wa Jamhuri ya Kiislamu na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) usiathiriwe na mtazamo na mwenendo usio thabiti na wenye migongano wa Washington.
-
Iran ni ya nne duniani kwa uzalishaji wa elimu katika uwanja wa mimea ya dawa
May 06, 2024 22:49Katibu wa Kamati ya Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ya Mimea ya Dawa na Tiba Asilia katika Ofisi ya Rais wa Iran ametangaza kuwa, watafiti wa Iran wanashika nafasi ya nne duniani katika uzalishaji wa sayansi katika uga wa uzalishaji wa mimea ya dawa na tiba asilia.
-
Utayari wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran wa kuendesha duru ya pili ya Uchaguzi wa Bunge
May 06, 2024 22:44Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran ametangaza utayarifu wa wizara hiyo wa kuendesha duru ya pili ya uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) siku ya Ijumaa ya tarehe 10 Mei.