-
Meja Jenerali Salami: Maadui wa Iran wameshindwa kuuangusha utawala wa Kiislamu
Dec 18, 2022 00:43Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) amesisitiza kuwa: Katika miaka ya karibuni maadui wote wameshindwa mkabala wa Mapinduzi ya Kiislamui, na vita na mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh ni miongoni mwa mifano ya kushindwa kwa adui.
-
Jenerali Ashtari: Maadui wa Iran ya Kiislamu wameshindwa kwa fedheha
Dec 17, 2022 07:39Mkuu wa Jeshi la Polisi la Iran amesisitiza juu ya ulazima wa kuegemea Jihadi ya ufafanuzi na kuweka wazi mambo katika vita vya simulizii na akasema: "Maadui wa Iran ya Kiislamu wameshindwa kwa fedheha katika makabiliano yao na wananchi."
-
Amir-Abdollahian: Utawala wa Israel ni tishio kubwa kwa usalama wa eneo
Dec 17, 2022 04:31Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema utawala wa Kizayuni ni utawala bandia, usio halali na ni tishio kubwa kwa usalama wa eneo.
-
Ayatullah Sayyid Muhammad Sadiq Rouhani aaga dunia
Dec 17, 2022 00:03Ayatullah Seyyed Muhammad Sadiq Rouhani, mmoja wa wanazuoni wa Chuo cha Kidini cha Qom, ameaga dunia usiku wa kuamkia leo.
-
Radiamali kali ya Iran dhidi ya kushadidi hatua za chuki za madola ya Magharibi
Dec 16, 2022 09:51Katika siku za hivi kariuni madola ya Magharibi yakiongozwa na Marekani yameshadidisha hatua na mashinikizo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yakitumia kama yanavyodai fursa ya kuibuka vurugu na machafuko hapa nchini.
-
Rais Raisi: Mahesabu ya adui katika njama ya karibuni yameenda kombo
Dec 16, 2022 08:30Rais Ebrahim Raisi amesema: kutokana na basira na kuwa macho wananchi wa Iran, mahesabu ya adui katika njama ya karibuni yameenda kombo sawa na ilivyokuwa katika fitna za huko nyuma.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Visiwa vitatu ni sehemu isiyotenganishika na ya milele ya Iran
Dec 16, 2022 08:30Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: "Visiwa vitatu ni sehemu isiyotenganishika na ya milele ya Iran ya Kiislamu. Sisi hatuna muhali na mtu yeyote kuhusu umoja wa ardhi yetu na tunachukua hatua bila mzaha".
-
Iran yapinga azimio la muswada wa Canada Baraza Kuu la UN
Dec 16, 2022 04:33Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amekutaja kupitishwa azimio la chuki dhidi ya Iran katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa pendekezo la Canada na kwa uungaji mkono wa nchi za Ulaya na utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni jambo linaloakisi unafiki na sera za kindumakuwili za nchi zilizopendekeza na kuunga mkono muswada wa azimio hilo.
-
Meja Jenerali Salami: Ndoto ya adui kuitawala Iran kamwe haitatimia
Dec 15, 2022 08:38Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema: Ndoto ya adui ya kutaka kuitawala Iran ya Kiislamu kamwe haitatimia, bali itaendelea kusalia tu kwenye akili yake ambapo atatumia nguvu zake zote kutaka kuifanikisha bila mafanikio yoyote.
-
Kan'ani Chafi: Azimio la Marekani dhidi ya Iran katika kikao cha ECOSOC halina hadhi ya kisheria
Dec 15, 2022 04:29Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali azimio lisilo na ridhaa ya wote la Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kikao cha Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC) na kulitaja kuwa ni hatua ya kisiasa, iliyokosa hadhi ya kisheria, iliyo kinyume na Hati ya Umoja wa Mataifa na yenye kuanzisha utaratibu mbaya katika taasisi hiyo ya kimataifa.