Amir-Abdollahian: Utawala wa Israel ni tishio kubwa kwa usalama wa eneo
Dec 17, 2022 04:31 UTC
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema utawala wa Kizayuni ni utawala bandia, usio halali na ni tishio kubwa kwa usalama wa eneo.
Ili kufikia malengo yao ya kujipanua, Wazayuni kila siku wanavamia na kushambulia maeneo mbalimbali ya Palestina na kuwaua shahidi na kuwajeruhi Wapalestina au kuwakamata na kuwaweka magerezani.
Kuhusiana na hili na kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hossein Amir-Abdollahian ameandika ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter akiashiria kwamba utawala bandia na haramu wa Israel ni ghasibu na mtenda jinai unaomiliki mamia ya vichwa vya nyuklia na akasisitiza kwa kusema: "Tel Aviv ni tishio kubwa kwa usalama wa eneo letu la pamoja".
Amir-Abdullahian ameongeza kuwa: bila ya shaka yoyote, mustakbali ni wa watu wa asili wa Palestina.

Siku chache zilizopita na katika ujumbe alioandika kwenye mtandao wa Twitter, Nasser Kan'ani Chafi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alizitaja Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kuwa ni wabeba dhima ya jinai za utawala wa Kizayuni kusisitiza kuwa: tawala hizo inapasa ziwajibike kwa kuwekwa kwenye kizimba cha washtakiwa.
Kanani aliandika: hakuna siku ambayo walimwengu hawasikii habari wa kuuawa shahidi, kujeruhiwa au kutekwa nyara watoto, chipukizi na vijana wa Kipalestina na utawala wa kibaguzi wa Kizayuni.
Kwa zaidi ya miaka 70 sasa haki za wananchi madhulumu wa Palestina zinaendelea kupondwa na kukanyagwa na utawala dhalimu wa Kizayuni wa Israel, huku viongozi wa utawala huo haramu wakizidi kuonyesha kiburi na jeuri kila uchao kutokana na kimya cha jumuiya za kimataifa.../
Tags