Meja Jenerali Salami: Maadui wa Iran wameshindwa kuuangusha utawala wa Kiislamu
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) amesisitiza kuwa: Katika miaka ya karibuni maadui wote wameshindwa mkabala wa Mapinduzi ya Kiislamui, na vita na mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh ni miongoni mwa mifano ya kushindwa kwa adui.
Meja Jenerali Hossein Salami amesema kuwa maadui wote duniani wamejitosa uwanjani na wameungana pamoja kukabiliana na taifa la Iran.
Huku akieleza kuwa, lengo la adui ni kuyaangamiza Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kwamba kuna ulazima wa kutambua kuwa hali ya sasa si ya kawaida, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amefafanua kuwa: Maadui wote duniani wameingia uwanjani dhidi ya taifa la Iran na kwamba hali hiyo ni inaonekana wazi na dhahiri.
Kamanda Mkuu wa IRGC amesema kuwa, Wazayuni, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Saudi Arabia pia zinaonekana katika uwanja wa kukabiliana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuongeza kuwa: Maadui wameuamini uwongo wanaousema wao wenyewe, na wao ndio watakaokuwa waathirika wa kwanza wa uongo huo.
Akizungumzia fitina iliyoanzishwa na madola ya kibeberu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu katika kipindi cha sasa, Meja Jenerali Hossein Salami ameashiria uwezo mkubwa wa dini ya Kiislamu wa kukabiliana na maadui na kusema: "Hii leo tunakidhi mahitaji yetu ya zana za kijeshi sisi wenyewe, na kama tusingewekewa vikwazo, tusingepata mafanikio na uwezo huu mkubwa."