-
Maduro wa Venezuela aisifu Iran kama mfano wa kupigania utawala wa sheria kimataifa
Dec 17, 2025 09:20Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, ameitaja Iran kuwa mfano bora duniani katika kutetea sheria za kimataifa, akishukuru Jamhuri ya Kiislamu kwa msimamo wake thabiti wa kuiunga mkono Caracas wakati ambapo vitisho kutoka Marekani vinaongezeka.
-
Kushtakiwa viongozi wa utawala wa Kizayuni; takwa la pamoja la mataifa ya Kiislamu
Dec 17, 2025 09:13Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amelaani jinai zinazoendelea kufanywa na Israel huko Ghaza na mashambulizi yake dhidi ya Lebanon, na amezitaka nchi za ukanda huu na jamii ya kimataifa ichukue hatua kali za kukabiliana na tishio la mara kwa mara la utawala wa Kizayuni dhidi ya amani na utulivu wa eneo hili na dunia nzima kwa ujumla.
-
Waziri wa Mambo ya Nje asisitizia tena azma ya Iran ya kutetea haki zake za kisheria za nyuklia
Dec 17, 2025 03:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi amesisitizia azma ya Jamhuri ya Kiislamu ya kutetea haki zake za kisheria za nyuklia kulingana na Mkataba wa Kuzuia Usambazaji wa Silaha za Nyuklia (NPT), akisema sera za nyuklia za Tehran zingali zinaendana na mfumo wa sheria za kimataifa.
-
Qalibaf asisitiza umuhimu wa utafiti katika kutatua matatizo ya kitaifa
Dec 16, 2025 23:21Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza umuhimu wa utafiti katika kutatua changamoto na matatizo ya kitaifa.
-
Baghaei: Jamii ya kimataifa ichukue hatua dhidi Israel
Dec 16, 2025 08:16Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani jinai zinazoendelea kufanywa na Israel huko Ghaza na mashambulizi yake dhidi ya Lebanon, na amezitaka nchi za ukanda huu na jamii ya kimataifa ichukue hatua kali za kukabiliana na tishio la mara kwa mara la utawala wa Kizayuni dhidi ya amani na utulivu wa eneo hili na dunia nzima kwa ujumla.
-
Iran yaitaka dunia izuie kuendelea mauaji ya Wapalestina Gaza
Dec 16, 2025 03:19Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei, amelaani vikali kuendelea kwa mauaji ya halaiki ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, akiashiria mashambulizi ya mabomu yanayoendelea kufanywa na Wazayuni na kuzuiwa kwa misaada ya kibinadamu.
-
Mauzo ya chai ya Iran nje ya nchi yaongezeka kwa 48%
Dec 16, 2025 03:12Mkuu wa Shirika la Chai la Iran, Habib Jahansaz amesema mauzo ya chai ya Jamhuri ya Kiislamu nje ya nchi katika miezi minane ya kwanza ya mwaka huu wa kalenda ya Iran (ulioanza Machi 21) yameongezeka kwa asilimia 48, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
-
Iran: Madai ya kumiliki visiwa vya Ghuba ya Uajemi ni dhidi ya mamlaka ya kujitawala na ujirani mwema
Dec 15, 2025 23:58Iran imesema kuwa madai yoyote ya kumiliki visiwa vitatu vya Ghuba ya Uajemi yaani Tomb Kubwa, TombNdogo na Bu Musa ni ukiukaji wa kanuni za ujirani mwema na kutoheshimu mamla ya kujitawala ya nchi nyingine.
-
Mkutano wa Tehran; Ubunifu wa Iran kwa ajili ya mwafaka wa kikanda na uthabiti wa Afghanistan
Dec 15, 2025 11:29Mkutano wa wawakilishi maalum wa nchi jirani za Afghanistan pamoja na Russia umefanyika katika wizara ya mambo ya nje ya Iran, mjini Tehran.
-
Iran: IAEA haina haki ya kutaka kukagua vituo vilivyoshambuliwa
Dec 15, 2025 08:05Mkuu wa shirika la nyuklia la Iran amekosoa wito wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA wa kufanya ukaguzi mpya kwenye maeneo ya nyuklia yaliyoshambuliwa, akisisitiza kwamba taasisi hiyo ya UN haina itifaki zilizo wazi za kukagua maeneo ambayo yalishambuliwa na utawala wa Israel na Marekani.