Jenerali Abdollahi: Jeshi la Iran litaendeleza mapambano ya kujihami hadi ushindi kamili
-
Meja Jenerali Ali Abdollahi
Kamanda wa Kamandi ya Khatam al‑Anbiya (SAW) katika Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika ujumbe wake kwamba: “Vikosi vyenye nguvu vya ulinzi vya Iran ya Kiislamu, kwa utiifu kamili kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, vimesimama imara katika ahadi yao ya kulinda taifa tukufu na lenye ushindi la Iran, na vitaendeleza njia hii tukufu kwa msaada wa watu wenye ufahamu na ushujaa wa Iran ya Kiislamu hadi ushindi kamili.”
Meja Jenerali Ali Abdollahi ameongeza kuwa: “Madola yaliyokuwa yakionekana kuwa na nguvu, hasa Marekani, ambayo kwa miongo mingi yamepora utajiri mataifa yaliyodhulumiwa duniani, hususan nchi za Kiislamu, kwa vitisho na hofu, sasa kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, yameshuhudiwa yakiporomoka mbele ya macho ya dunia. Baada ya kushindwa kwa fedheha katika jitihada zao za kuunda muungano dhidi ya Iran ya Kiislamu, leo wanatafuta njia ya kutoroka na kujinasua kutoka kwenye vita ambayo wao wenyewe waliianzisha.”
Jenerali Abdollahi ameongeza kuwa: “Rais Donald Trump wa Marekani, baada ya kutambua hali halisi ya uwanda wa vita na kujikuta amenaswa katika kinamashi cha vita, na baada ya kukata tamaa kufikia malengo yake, sasa amewageukia viongozi wa baadhi ya nchi kutafuta njia ya kutoka kwenye vita. Hali hii ya kihistoria ni heshima kubwa kwa taifa shujaa la Iran.”
Mwisho wa ujumbe wake, Jenerali Abdollahi ameandika hivi: “Katika hatua hii nyeti ya vita, vikosi vyenye nguvu vya ulinzi vya Iran ya Kiislamu, kama vilivyomuahidi Imam shahidi wa Ummah, vimesimama imara katika ahadi yao ya kulilinda taifa tukufu na lenye ushindi la Iran. Hivi sasa kwa utiifu kamili kwa Kiongozi wetu mpenzi na Amiri Jeshi Mkuu, Imam Sayyid Mojtaba Khamenei, vikosi hivi vitaendeleza njia hii tukufu kwa msaada wa watu wenye ufahamu na ushujaa wa Iran ya Kiislamu hadi kufikia ushindi kamili.”