Msemaji wa Jeshi la Iran: Msiite kushindwa kuwa ni makubaliano
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137564-msemaji_wa_jeshi_la_iran_msiite_kushindwa_kuwa_ni_makubaliano
Msemaji wa Kamandi ya Khatamul Anbiya (SAW) ya Jeshi la Iran amewahutubu watawala wa Marekani na kuwaambia kuwa, wasiite kushindwa kuwa ni makubaliano.
(last modified 2026-03-25T04:57:27+00:00 )
Mar 25, 2026 04:57 UTC
  • Kanali Ibrahim Dhulfiqari
    Kanali Ibrahim Dhulfiqari

Msemaji wa Kamandi ya Khatamul Anbiya (SAW) ya Jeshi la Iran amewahutubu watawala wa Marekani na kuwaambia kuwa, wasiite kushindwa kuwa ni makubaliano.

Kanali Ibrahim Dhulfiqari  amesema, Amesema wanaodai kuwa dola lenye nguvu zaidi duniani, lau wangeweza  kujinasua kutoka kwenye mgogoro walioingia wangefanya hivyo muda mrefu uliopita.

Ameendelea kusema: “Msiite kushindwa kwenu kuwa ni makubaliano. Kipindi cha ahadi zenu kimeshaisha. Leo duniani kuna kambi mbili tu: ya haki na ya batili. Na kila mtu mpenda‑haki na aliye huru, hatadanganywa na mawimbi ya upotoshaji wa vyombo vyenu vya habari.

Halikadhalika amesema: Hakutakuwa na uwekezaji wenu katika eneo, wala hamtashuhudia tena bei za zamani za nishati na mafuta hadi pale mtakapotambua kuwa: utulivu wa eneo hili unahakikishwa kwa mkono wenye nguvu wa vikosi vya ulinzi vya Iran.”

 Halikadhalika amesema hakuna hali yoyote itakayorudi kama ilivyokuwa zamani na kwamba mapambano yataendelea hadi pale dhana ya kuchukua hatua dhidi ya taifa la Iran itakapofutika kikamilifu kutoka katika fikra chafu za adui.

Msemaji huyo wa Jeshi la Iran pia amewafahamisha wafamizi kuwa wanafanya makosa kufananisha vita vyao na taifa lenye ghera na jeshi imara la Iran na filamu za Hollywood na mashujaa za kidhahania na wa kubuni akilini, na mumeanzisha uchokozi kutokana na makosa ya kimahesabu.

Hivi karibuni Rais wa Marekani alilazimika kuondoa vitisho vyake kuhusu kushambulia miundombinu ya umeme ya Iran baada ya onyo kali la Iran.

Baada ya Tump kutoa tishio la kulenga miundombinu ya nishati ya Iran ndani ya saa 48, Iran ilitoa onyo kwamba iwapo vitisho hivyo vingetekelezwa, mashambulizi dhidi ya miundombinu ya umeme na miundombinu muhimu ya utawala wa Kizayuni na ya Marekani katika eneo hili ingelengwa na kuharibiswa kikamilifu na vikosi vya ulinzi vya Iran.

Katika ujumbe alioweka kwenye mtandao wake wa kijamii, Trump aliandika kuwa ameagiza kuahirishwa kwa mashambulizi yote yaliyopangwa dhidi ya miundombinu ya nishati ya Iran kwa muda wa siku tano. Aidha, alidai kuwa yuko katika mazungumzo na Iran ili kufikia mapatano ya kumaliza vita alivyoanzisha.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekanusha madai ya kuwepo mazungumzo yoyote baina ya Iran na Marekani katika siku 24 za hivi karibuni za vita vya kulazimishwa.