Aragchi: Iran itaendeleza mapambano dhidi ya maadui
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137584-aragchi_iran_itaendeleza_mapambano_dhidi_ya_maadui
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi, ametilia mkazo uamuzi wa Jamhuri ya Kiislamu kuendelea na sera ya Muqawama na mapambano dhidi ya wavamizi.
(last modified 2026-03-26T07:35:47+00:00 )
Mar 26, 2026 04:34 UTC
  • Aragchi: Iran itaendeleza mapambano dhidi ya maadui

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi, ametilia mkazo uamuzi wa Jamhuri ya Kiislamu kuendelea na sera ya Muqawama na mapambano dhidi ya wavamizi.

Katika mahojiano na kanali ya habari ya Iran, Araghchi amesema. “Kwa sasa, sera yetu ni kuendeleza mapambano.”

Amesisitiza kuwa, “Kwa sasa hakuna mazungumzo yanayoendelea,” huku akihoji pia uaminifu wa ahadi za adui.

Kwa mujibu wa Press TV, mawasiliano ya kidiplomasia kuhusu mazungumzo ya kumalizika vita yamekuwepo katika ngazi ya kikanda, lakini msimamo wa Tehran bado haujabadilika.

Waziri Araghchi pia amesema kuwa “dhamana za kimataifa si za kuaminika kwa asilimia mia moja,” akiashiria juhudi zinazoripotiwa za baadhi ya nchi za tatu kujaribu kuwa wapatanishi ili kumaliza uchokozi usio halali ulioilazimisha Jamhuri ya Kiislamu kujibu kwa hatua madhubuti.

Amesema Iran yenyewe sasa inachukua hatua za kujiwekea dhamana ili kuhakikisha hakuna atakayethubutu tena kuanzisha vita dhidi ya watu wa Iran. Araghchi alikuwa akiashiria hatua za kulipiza kisasi za Iran ambapo vikosi vya ulinzi vya Iran vimetekeleza angalau mawimbi 81 ya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya malengo nyeti na ya kimkakati ya Marekani na Israel katika eneo.

Araghchi amebainisha kuwa: “Usitishaji mapigano bila dhamana ni mzunguko hatari unaoishia kurudia vita tena,” na kuongeza kuwa: “Adui lazima apate funzo la kudumu, ili kamwe asifikirie tena kuanzisha shambulio jingine, na madhara yaliyowapata watu wa Iran lazima yafidiwe.”

Araghchi amesema matukio ya hivi karibuni yameonyesha wazi kuwa kuruhusu Marekani kuanzisha vituo vya kijeshi katika ardhi za nchi za eneo hili kunahatarisha usalama wa nchi hizo badala ya kuimarisha usalama wao.

Alikuwa akiashiria hatua ya Iran kushambulia  vituo vya  jeshi la kigaidi la Marekani katika nchi za Kiarabu za eneo la Magharibi mwa Asia kama Qatar, Bahrain, Kuwait, Saudi Arabia na Jordan. Vituo hivyo vimekuwa vikitumiwa na Marekani na Israel katika kutekeleza mashambulizi ya kichokozi dhidi ya Iran.

Araghchi amesema kwamba baadhi ya nchi za eneo hilo hapo awali zilisema hazitaruhusu ardhi zao kutumiwa dhidi ya Iran, lakini baadaye kauli hizo hazikuzingatiwa.

Araqhchi amesema adui ameshindwa kufikia malengo kadhaa, ikiwemo kugawanya nchi, kupata ushindi wa haraka, na kudhoofisha mshikamano wa ndani wa Iran.

Kuhusu Lango Bahari la Hormuz, ambao Iran imeliufunga kwa maadui na washirika wao tangu kuanza kwa uchokozi mwishoni mwa mwezi uliopita, Araqhchi amesema njia hiyo ya kimkakati bado iko wazi kwa nchi rafiki. Amesema, “Kwa baadhi ya nchi tulizozitambua kuwa marafiki, tuliruhusu meli zao kupita katika Lango Bahari la Hormuz. Nchi hizo ni pamoja na China, Russia, India, Iraq na Pakistan. Amesema Iran haina sababu ya kuruhusu maadui wake kupita katika njia hiyo muhimu ya bahari duniani.