-
Raisi: Marekani inapaswa kufanya uamuzi kuhusu mazungumzo ya nyuklia
Oct 25, 2022 04:47Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran imeeleza hoja zake kwa mantiki na kusema kuwa, Marekani inapaswa kufanya uamuzi kuhusu mazungumzo ya nyuklia.
-
Raisi: Ushirikiano mzuri na taasisi za kikanda ni kipaumbele cha sera za kigeni za Iran
Oct 24, 2022 22:56Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kuwa, Tehran imekuwa ikishirikiana vyema katika nyakati tofauti na Jumuiya ya Nchi za Pambizoni mwa Bahari ya Hindi; na kwamba kushirikiana vyema na taasisi za kikanda ni kipaumbe cha sera za kigeni za Iran.
-
Watu 10 watiwa nguvuni nchini Iran kwa tuhuma za kushirikiana na MOSSAD
Oct 24, 2022 22:55Kitengo cha Habari cha Idara ya Mahakama ya Iran kimetangaza kutiwa nguvuni watu 10 kwa tuhuma za kushirikiana na shirika la ujasusi la Israel (MOSSAD).
-
Kan'ani: Inachotaka Iran katika mazungumzo ni haki yake ya kisheria, ya wazi na ya kimantiki
Oct 24, 2022 09:12Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, inachotaka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia ni haki zake za kimsingi, za kisheria, za wazi na za kimantiki. Inachotaka ni kuondolewa vikwazo iliivyowekewa kidhulma na mabeberu.
-
China yapinga vikwazo haramu na vya upande mmoja vya EU dhidi ya Iran
Oct 24, 2022 00:31China imepinga na kukosoa vikali hatua ya Umoja wa Ulaya ya kuiwekea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vikwazo ilivyovitaja kuwa haramu na vya upande mmoja.
-
Iran: Ulimwengu wa Kiislamu unakabiliwa na ugaidi wa vyombo vya habari
Oct 23, 2022 09:20Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu wa Iran amesema, vyombo vya habari vyenye uadui vinapindua ukweli na kuandaa habari bandia ili kujaribu kutoa taswira isiyo sahihi kuhusu Iran ya Kiislamu na Ulimwengu wa Kiislamu.
-
Teleskopu mpya ya Iran yawashangaza wengi duniani + Video
Oct 23, 2022 04:36Katika hatua kubwa kwa jumuiya ya wanasayansi ya Iran, wanaastronomia wa Kituo cha Kitaifa cha Uangalizi wa Anga za Mbali cha Iran (INO) wameweza kupata mafanikio makubwa.
-
Amir-Abdollahian: Mienendo ya Marekani ni ya kinafiki
Oct 23, 2022 01:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa viongozi wa Marekani wanazungumza jambo moja na kutenda vingine, na mara nyingi hutafuta hutaka kujionesha mbele ya vyombo vya habari.
-
Barua ya Troika ya Ulaya kwa Umoja wa Mataifa: Mwendelezo wa vita vya kisiasa na kipropaganda dhidi ya Iran
Oct 22, 2022 23:05Katika barua yake kwa Umoja wa Mataifa, Troika ya Umoja wa Ulaya inayojumuisha Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, imekariri madai ambayo hayajathibitishwa kwamba Russia inatumia ndege zisizo na rubani zilizotengenezwa na Iran katika vita vya Ukraine, na imeutaka Umoja wa Mataifa kuchunguza iwapo huo ni ukiukaji ya Azimio 2231 la Baraza la Usalama au la
-
Iran: Hatutaipatia Marekani fursa yoyote ya ziada katika mazungumzo ya uondoaji vikwazo
Oct 22, 2022 09:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, Iran inachukua hatua kwa kutumia mantiki na kuchunga mistari myekundu ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na haitapatia Marekani fursa yoyote ya ziada katika mazungumzo ya uondoaji vikwazo.