Oct 24, 2022 04:01 UTC
  • China yapinga vikwazo haramu na vya upande mmoja vya EU dhidi ya Iran

China imepinga na kukosoa vikali hatua ya Umoja wa Ulaya ya kuiwekea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vikwazo ilivyovitaja kuwa haramu na vya upande mmoja.

Katika kikao na waandishi wa habari, Wang Wenbin, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema, "China inapinga uwekaji wa vikwazo haramu na vya upande mmoja bila kulihusisha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na bila kuzingatia misingi ya sheria za kimataifa."

Wenbin alikuwa akijibu swali la mwandishi wa habari wa shirika la habari la TASS, aliyetaka kujua radiamali ya Beijing baada ya EU kuwawekea vikwazo makamanda watatu waandamizi wa Jeshi la Iran na kampuni ya Kiirani ya kuzalisha ndege zisizo na rubani.

EU ilitangaza vikwazo hivyo dhidi makamanda na kampuni za droni ya Iran kwa madai kwamba, Russia inatumia ndege zisizo na rubani zilizotengenezwa na Jamhuri ya Kiislamu katika vita vya Ukraine. 

Katika barua yake kwa Umoja wa Mataifa, Troika ya Umoja wa Ulaya inayojumuisha Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, ilikariri madai ambayo hayajathibitishwa kwamba Russia inatumia droni zilizotengenezwa na Iran katika vita vya Ukraine, na kuutaka Umoja wa Mataifa kuchunguza iwapo huo ni ukiukaji ya Azimio 2231 la Baraza la Usalama au la.

Troika ya Ulaya

Hata hivyo Amir-Saeid Iravani, Mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amekanusha madai hayo ya Ukraine kwamba Jamhuri ya Kiislamu ilikiuka Azimio la Umoja wa Mataifa kwa kile Kiev inachodai kuwa eti kuipatia Russia ndege zisizo na rubani au drone.

Akijibu madai ya Ukraine, Iravani alibainisha kuwa vikwazo vilivyotajwa katika azimio hilo la Baraza la Usalama "vilimalizika Oktoba 2020." Aliongeza kuwa tangu wakati huo, Iran haijakuwa chini ya vikwazo vya , uuzaji au uhamishaji wa silaha kwa nchi zingine.

Tags