Amir-Abdollahian: Mienendo ya Marekani ni ya kinafiki
(last modified Sun, 23 Oct 2022 04:34:23 GMT )
Oct 23, 2022 04:34 UTC
  • Amir-Abdollahian: Mienendo ya Marekani ni ya kinafiki

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa viongozi wa Marekani wanazungumza jambo moja na kutenda vingine, na mara nyingi hutafuta hutaka kujionesha mbele ya vyombo vya habari.

Amir Abdollahian jana Jumamosi alitembelea shule za Wairani huko Yerevan mji mkuu wa Armenia na kukutana na Wairani wanaoishi nchini humo. Abdollahian aliashiria kukinzana kwa mienendo ya viongozi wa Marekani mkabala wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema: Tehran haitatoa mwanya kwa viongozi wa Marekani kuenea ghasia na fujo ndani ya Iran kwa kutuma jumbe na wakati huo huo wanadai eti wanataka kufanya mazungumzo na Iran. 

Amir-Abdollahian amesisitiza kuwa fikra za waliowengi zinahitaji upashaji habari makini. Amesema, kiongozi mmoja wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani anaitangazia Iran kwamba, nchi hiyo ina wasiwasi kuhusu suala la kufikiwa mapatano lakini ni anatangaza mbele ya vyombo vya habari kuwa, mazungumzo si kipaumbele cha kwanza cha Washington. Amesema, mwenendo huo wa Marekani ni wa kinafiki.

Kuhusu mapigano kati ya Armenia na Jamhuri ya Azerbaijan juu ya mzozo wa Nagorno-Karabakh, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: "Iran haitaki kuona vikosi vya majeshi ya nchi ajinabi vikiingilia kivyovyote katika mzozo huo.

Nagorno-Karabakh

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga vita katika maeneo yote duniani hasa kati ya Russia na Ukraine na Armenia na Jamhuri ya Azerbaijan.