-
Ujumbe wa Rambirambi wa Kiongozi Muadhamu Kufuatia kuuawa shahidi Dkt.Larijani
Mar 19, 2026 05:30Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei, ammetuma ujumbe wa rambirambi kufuatia kuuawa shahidi kwa Dk. Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, pamoja na mwanawe na baadhi ya wenzake.
-
Siku ya ishirini ya mapambano; Wazayuni na Wamarekani watenda jinai katika kinamasi
Mar 19, 2026 03:55Vita vya kichokozi vilivyoanzisha na Marekani kwa kushirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, sasa vimeingia siku yake ya ishirini.
-
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran: Tutalipiza kisasi kwa damu ya Shahidi Larijani
Mar 18, 2026 06:25Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Luteni Jenerali Hatami amesema kuwa jibu la Iran kwa mauaji ya kigaidi ya Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa litakuwa thabiti na la kuwafanya wahusika wajute.
-
Iran yatuma barua UN; yalalamikia mashambulizi ya US dhidi yake kutokea katika nchi za eneo
Mar 18, 2026 05:51Iran imetuma barua saba tofauti kwa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo kuhusiana na mashambulizi ya Marekani dhidi yake kutokea katika nchi za kanda hii.
-
Iran yamnyonga jasusi wa shirika la ujasusi la Israel, Mossad
Mar 18, 2026 05:05Mahakama ya Iran imetangaza mapema Jumatano kwamba imemnyonga mtu aliyepatikana na hatia ya kufanya ujasusi kwa maslahi ya utawala haramu wa Israel.
-
Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, ameuawa Shahidi
Mar 18, 2026 03:43Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetangaza kuuawa shahidi kwa katibu wake, Ali Larijani, kufuatia shambulio la maadui, ambao ni Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Araqchi amwambia Guterres: Simamisheni uchokozi wa Marekani na Israel dhidi ya Iran
Mar 17, 2026 08:43Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: "Matatizo ya usafirishaji wa meli katika Mlango-Bahari wa Hormuz ni matokeo ya vita vilivyoanzishwa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, na kila nchi au shirika la kimataifa linalojali amani na usalama lazima lilaani uhalifu wa tawala hizo mbili na kutoa wito wa kukomeshwa uchokozi wao wa kijeshi dhidi ya taifa la Iran."
-
Araqchi: Vita vitaisha kwa njia itakayomfanya adui asifikirie tena kutushambulia
Mar 17, 2026 07:01Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu haijatuma ujumbe wa aina yoyote kwa wavamizi wala haijaomba kusitishwa vita.
-
Pezeshkian: Iran haitasalimu amri mbele ya madola ya kibeberu
Mar 17, 2026 06:04Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema taifa hili halitasalimu amri kamwe mbele ya madola ya kibeberu, huku akiitaka jamii ya kimataifa kulaani uvamizi wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Iran yazitaka nchi za Kiislamu zitangaze msimamo, yasema Marekani haiaminiki
Mar 17, 2026 04:45Katika taarifa yenye vipengele sita iliyoelekezwa kwa serikali za nchi za Kiislamu, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema: “Lazima muamue msimamo wenu katika Vita vya Ramadhani, je, mnasimama upande wa nchi ya Kiislamu ya Iran, au upande wa Marekani na Israel?”