Iran yamnyonga jasusi wa shirika la ujasusi la Israel, Mossad
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137436-iran_yamnyonga_jasusi_wa_shirika_la_ujasusi_la_israel_mossad
Mahakama ya Iran imetangaza mapema Jumatano kwamba imemnyonga mtu aliyepatikana na hatia ya kufanya ujasusi kwa maslahi ya utawala haramu wa Israel.
(last modified 2026-03-18T05:05:00+00:00 )
Mar 18, 2026 05:05 UTC
  • Kourosh Keyvani
    Kourosh Keyvani

Mahakama ya Iran imetangaza mapema Jumatano kwamba imemnyonga mtu aliyepatikana na hatia ya kufanya ujasusi kwa maslahi ya utawala haramu wa Israel.

Hukumu ya kifo dhidi ya jasusi huyo wa Israel ambaye alikuwa akituma picha na taarifa za maeneo nyeti nchini Iran kwa maafisa wa Mossad, imetekelezwa baada ya kufuata utaratibu wa kisheria na kuidhinishwa na Mahakama Kuu.

Kourosh Keyvani alitambuliwa na kukamatwa na Shirika la Ujasusi la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) katika jumba moja kwenye mji wa Savjbolagh Juni 16 mwaka huu, siku ya nne ya Vita vya Siku 12, akiwa na euro 30,000 pesa taslimu, gari la kubebea mizigo aina ya Padra, pikipiki na vifaa mbalimbali vya kisasa vya ujasusi na mawasiliano ya setalaiti.

Baada ya miaka miwili ya mafunzo ya aina mbalimbali kutoka kwa maajenti wa Mossad katika miji mikuu ya Austria, Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji, Denmark, Slovakia na Israel, Kourosh Keyvani alitumwa Iran kufanya shughuli za ujasusi kwa maslahi ya utawala huo haramu.

Katika miezi ya hivi karibuni, mamlaka husika za Iran zilifanya operesheni kadhaa za kuwakamata na kuwanyongwa watu waliopatikana na hatia ya kufanya ujasusi hapa nchini kwa maslahi ya Marekani na Israel.

Itakumbukwa kuwa Oktoba mwaka jana, Bunge la Iran lilipitisha sheria mpya inayoongeza adhabu kali kwa wale wanaotuhumiwa kushirikiana na mashirika ya ujasusi ya kigeni, hasa yale ya Marekani na Israel.