-
Iran yazidi kuimarisha biashara na nchi za Afrika
Jun 08, 2022 22:36Naibu mkuu wa Shirika la Kukuza Biashara la Iran (TPO) anayeshughulikia maendeleo ya masoko ya nje amesema shirika lake linatafuta njia za kutekeleza mifumo ya biashara ya kubadilishana bidhaa na washirika wa kibiashara wa bara la Afrika.
-
Kiongozi Muadhamu: Kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel kutapelekea kudhalilika madola ya Kiarabu
Jun 08, 2022 07:22Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema tawala za Kiarabu zilizokhitari kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel bila ridhaa ya wananchi wao hazitakumbwa na hatima nyingine ghairi ya kuishia kudhalilishwa na kutumiwa vibaya na utawala huo haramu.
-
Jenerali: Tutateketeza Tel Aviv, Haifa iwapo Israel itafanya kosa dhidi ya Iran
Jun 08, 2022 06:19Kamanda wa vikosi vya nchi kavu vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonya kuwa, Tehran itaiteketeza miji ya Tel Aviv na Haifa iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utajaribu kufanya kosa lolote dhidi ya taifa hili.
-
Watu 17 waaga dunia katika ajali ya treni ya abiria Iran
Jun 08, 2022 03:22Kwa akali watu 17 wameaga dunia na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia ajali ya treni ya abiria iliyotokea mapema alfajiri ya leo hapa nchini Iran.
-
Mtaalamu wa zamani wa UN: Hatua ya Israel kumuua kanali wa IRGC ni ugaidi wa kiserikali
Jun 07, 2022 06:57Mhadhiri Mmarekani katika taaluma ya sheria za kimataifa ambaye aliwahi kuwa ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa amesema mauaji yaliyotekelezwa na utawala wa Israel dhidi ya afisa wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) mwezi uliopita yalikuwa ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa, na kusema kwa mauaji hayo, Israel ina hatia ya "ugaidi unaofadhiliwa na serikali."
-
Spika: Mapinduzi ya Kiislamu Iran yalitokana na fikra za Umahdi na Ashura
Jun 07, 2022 06:45Spika wa Bunge la Iran amesema chimbuko la Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni fikra za Imam Mahdi, Mwenyezi Mungu Aharikishe Kudhihiri Kwake, na Ashura.
-
Iran yasikitishwa na shambulio la kigaidi lililoua makumi Nigeria
Jun 07, 2022 03:39Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani shambulio la kigaidi lililoua makumi ya watu kanisani huko Nigeria hivi karibuni, sanjari na kutoa mkono wa pole kwa serikali ya Abuja na familia za raia wa nchi hiyo ambao waliuawa katika hujuma hiyo.
-
Abdollahian: Iran itaendelea kuunga mkono muqawama wa Palestina
Jun 06, 2022 23:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu katu haitoruhusu kukanyagwa haki za Wairani katika mazungumzo (ya Vienna) au kupuuza haki za wananchi Waislamu wa Palestina na kueleza bayana kuwa, Tehran itaendelea kuunga mkono muqawama wa Wapalestina.
-
Iran: Tutachukua hatua zinazofaa kukabiliana na hatua za kiadui za IAEA
Jun 06, 2022 22:02Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, muswada wa azimio la Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA kwa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa haikubaliki kabisa na kwamba Tehran itajibu inavyofaa hatua hiyo ya IAEA.
-
Sisitizo la Waziri wa Uchumi na Fedha wa Iran kuhusu kushirikiana nchi za Kiislamu kwa ajili ya kuimarisha uchumi.
Jun 06, 2022 05:38Akizungumza Jumamosi katika kikao cha kila mwaka cha Baraza Kuu la Benki ya Maendeleo ya Kiislamu IDB huKo mjini Cairo Misri, Ehsan Khandouzi, Waziri wa Masuala ya Kiuchumi na Fedha wa Iran, amesisitiza juu ya ulazima wa nchi za Kiislamu kushirikiana kwa ajili ya kuimarisha uthabiti wa kiuchumi wa nchi hizo na kuufanya kuwa na misingi madhubuti zaidi katika kukabiliana na changamoto zilizopo na za baadaye.